Ticker

6/recent/ticker-posts

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA MAWAKALA WA FORODHA YAKAMILIKA

Katika kuhakikisha taifa linapata viongozi bora wa kesho, taasisi zisizo za kiserikali za HakiElimu na The African Leadership Initiative For Impact (ALI For Impact) zimezindua programu maalum ya kuwawezesha vijana walioko mashuleni kupata maarifa na ujuzi wa uongozi.

Mpango huu mpya unalenga kuwa chachu ya mabadiliko kwa kuwapa wanafunzi nafasi ya kutambulika, kuendelezwa na hatimaye kuchukua nafasi kama viongozi wa baadaye katika sekta mbalimbali zenye uhitaji mkubwa wa uongozi thabiti na wenye maadili.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam mapema leo, Makumba Munezi, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uvumbuzi na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, alisema kuwa programu hiyo imeanzishwa baada ya kubainika mapungufu makubwa katika maandali… 🚨🌏HakiElimu na ALI For Impact Waibuka na Mpango Kuibua Viongozi Chipukizi Mashuleni 👇🏻👇🏻 https://www.okuly.co.tz/2025/04/hakielimu-na-ali-for-impact-waibuka-na.html Asante Pamoja Mwamba

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Mawakala wa Fordha yamekamilika huku viongozi wa sekta mbalimbali wakitarajiwa kushiriki katika kujadili njia bora za kuimarisha mifumo ya forodha na kuhimiza biashara ya kimataifa. Mkutano huo, unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 30 April mpaka tarehe Mosi Mei,2025 kwenye Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar , utaangazia masuala ya teknolojia ya kisasa katika forodha, uwazi wa mchakato wa biashara, na mikakati ya kudhibiti magendo.

Akizungumza na Wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar Mhe Idrissa Kitwana Mustapha ametoa pongezi kwa kamati za maandalizi kutoka Tanzania Bara na Visiwani kwa kazi nzuri na kuhimiza washiriki kutumia fursa hiyo kujenga ushirikiano imara na kuleta mapendekezo yatakayoharakisha maendeleo ya sekta ya forodha nchini.

Mkutano huu unatarajiwa kuvutia wadau zaidi ya 500 kutoka sekta za umma na binafsi, pamoja na washirika wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

0 Comments