Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Taasisi ya HolySmile imeandika historia mpya katika sekta ya maendeleo ya kijamii kwa kuandaa kwa mafanikio makubwa Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za Mdau Shupavu – Msimu wa Kwanza, tukio ambalo limefanyika usiku wa Mei 25, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwanza Hotel Jijini Mwanza.
Tukio hilo, ambalo lilikusudia kutambua, kuthamini na kuhamasisha mchango wa watu binafsi, taasisi na makundi mbalimbali katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kitamaduni, limehudhuriwa na viongozi wa serikali, wawakilishi wa taasisi za umma na binafsi, wadau wa maendeleo kutoka sekta mbalimbali, waandishi wa habari pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti nchini.


0 Comments