Ikiwa ni zawadi mpya kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva, Mugga Mo amekuja kivingine kwenye ngoma mpya inayobeba jina la "Kama Wao", akimshirikisha Bando MC.
Ngoma hii mpya imeachiwa rasmi na tayari inafanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na YouTube.
Hii ni kazi iliyopikwa na maprodyuza wawili wenye mikono ya dhahabu – Prez Beatz na Jay Drama– chini ya studio ya @skiasound, huku video kali ikiongozwa na director anayekuja juu kwa kasi, @iamblaxx.
"Kama Wao" si ngoma ya kawaida. Ina ujumbe mzito wa kujiamini mafanikio, na harakati za maisha ya mtaani. Midundo ni tamu, mashairi ni moto, na vibe yake ni ya kurudia rudia bila kuchoka!
Mugga Mo na Bando MC wameonesha kuwa wanajua wanachokifanya.
Ngoma hii inatoa nafasi kwa mashabiki kusafiri kisaikolojia kutoka mitaa hadi jukwaa la ushindi.
Usiache kusikiliza Ngoma hii kali!
0 Comments