Ticker

6/recent/ticker-posts

Watendaji wa Uchaguzi waaswa kufuata sheria, Kanuni, miongozo na taratibu za Uchaguzi.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira, leo Julai 15, 2025, wakati akifungua mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi Mkuu ngazi ya Mkoa na Jimbo kwa Mkoa Tabora na Kigoma, huku akiwaasa watendaji hao kufuata Sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao.

"Someni kwa umakini katiba, Sheria, Kanuni, miongozo na Maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume na ulizieni ili mpate kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine kutakuwa na changamoto" alisema Mhe.Rwebangira.

Mhe.Rwebangira aliwasisitiza kujiepusha kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi sambamba na kuajiri watendaji wa vituo wenye weledi, wanaojitambua,wazalendo, waadilifu na wachapakazi huku wakiachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za Uchaguzi.

Mafunzo haya ya siku tatu yanatarajia kukamilika tarehe 17 Julai, 2025 huku yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo watendaji wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa

Post a Comment

0 Comments