Na Halfan Chusi, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Agnes Meena, amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wafugaji wanguruwe ni pamoja na ugonjwa wa homa ya nguruwe, gharama za chakula, na kukosekana kwa masoko ndani na nje ya nchi.
Agnes ameyasema hayo leo Septemba 11 katika kongamano maalumu lililo wakutanisha wafugaji wa nguruwe na wadau wa sekta hiyo ndani na nje ya nchi.
Amesema sekta ya nguruwe kwa Sasa inakuwa kwa kasi na imechangia vijana wengi kupata ajira na kwamba idadi ya wafugaji wa nguruwe kwa Sasa Afrika inazidi Milioni 4.
Amesema kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo sambamba na kuweka mikakati ya kuondoa ugonjwa huo alioutaja kama ni kikwazo kikubwa kwa wafugaji.
Aidha amesema mkutano huo utawasaidia wafugaji nchini kujenga ukaribu na wale wa nje ya nchi pamoja na kubadilishana uzoefu utakao wasaidia kuboresha ufugaji wao.
"Serikali kazi yetu kutoa huduma, tafiti, tiba, na kuwawezesha wakulima na wengine kwaajili kupata masoko" amesema
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafugaji wa Nguruwe Tanzania, Doreen Maro amesema sekta ya ufugaji wa wanyama hao inakuwa kwa kasi kutokama na upatikanaji mbegu nzuri ambazo ni matokeo ya jitihada za jumuiya hiyo.
Amewataka watu mbalimbali ikiwamo wastaafu na vijana kujitosa katika ufugaji wa nguruwe akisisitiza unalipa na ni biashara nzuri.
Mfugaji wa Nguruwe, Ziaka Lameki ameshukuru kongamano hilo kujadili kuhusu namna ya kukabili changamoto zinazoikabili sekta hiyo akitamba Sasa ataweza kufuga kisasa na kupata matokeo makubwa.

0 Comments