Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akikabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jitihada za kuipeleka sekta ya ushirika kwenye mfumo wa kidijitali mkoani Shinyanga zimepata msukumo mpya, baada ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU LTD 1984) kukabidhi kompyuta mpakato 50 kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50 vilivyofanya vizuri katika mwaka wa fedha 2024/2025, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuendesha ushirika kwa mfumo wa kidijitali.
Kompyuta hizo zimekabidhiwa leo Jumatatu Desemba 15, 2025, wakati wa mafunzo maalum ya TEHAMA na uendeshaji wa ushirika yanayofanyika katika Ukumbi wa Lyakale, Manispaa ya Shinyanga, (Desemba 15-17,2025) yakihusisha viongozi wa AMCOS kutoka kanda mbalimbali za mkoa huo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, ameipongeza SHIRECU kwa kutoa vifaa vya TEHAMA na kuendelea kuliwekea mkazo eneo la mafunzo, akisisitiza kuwa mafunzo ni msingi muhimu wa maendeleo ya ushirika.
“Ushirika unaendeshwa kwa misingi na sheria zake. Tukiziacha, ushirika unakufa au unakwenda vibaya. SHIRECU endeleeni kuvilea vyama hivi na kuviweka karibu,” amesema Mtatiro.
Ameongeza kuwa ufufuaji wa SHIRECU unapaswa kuwa endelevu, akieleza kuwa changamoto zilizopo zinaweza kurekebishwa na historia ya chama hicho iwe chachu ya kusonga mbele, sambamba na kulinda amani na usalama wa nchi.
Kwa upande wake, Mrajis Msaidizi wa Ushirika Mkoa wa Shinyanga, Ibrahim Kakozi, amesema ugawaji wa kompyuta umeanza na vyama 50 vilivyofanya vizuri, huku mpango ukiwa ni kufikia AMCOS zote 107 zilizopo mkoani humo ili kuhakikisha ushirika unajiendesha kwa mifumo ya kisasa ya kidijitali.
Amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kujenga uwezo na uelewa wa viongozi wa AMCOS, ili kuboresha utendaji wao na kuendana na mahitaji ya sasa ya ushirika wa kisasa.
“Tunataka Shinyanga iendeshe ushirika kidijitali. Kompyuta hizi ni nyenzo muhimu za kutunza taarifa sahihi, kuleta uwazi na kurahisisha kazi za kila siku,” amesema Kakozi.
Naye Meneja Mkuu wa SHIRECU, Alpha Makasi, amesema mafunzo hayo yamelenga Wenyeviti na Makatibu wa AMCOS kutoka kanda za Uzogore, Mhunze na Solwa, yakijikita katika matumizi ya mifumo ya uendeshaji, utunzaji wa vitabu vya hesabu, maadili na misingi ya ushirika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya SHIRECU, Naomi Mayega Chaba, amesema matumizi ya mfumo wa kidijitali yataondoa changamoto zilizokuwepo awali za matumizi ya karatasi, ikiwemo kupotea kwa kumbukumbu na taarifa muhimu za wanachama.
Aidha, Mkaguzi wa Ndani wa SHIRECU, Joseph Bukombe, amesisitiza umuhimu wa maadili, uwajibikaji na utunzaji wa fedha, akionya kuwa baada ya mafunzo hayo, kiongozi atakayeshindwa kuwa na taarifa sahihi hatafaa kuendelea kuongoza ndani ya ushirika.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo yamewasaidia kuelewa kwa kina masuala ya maadili na uwajibikaji, huku wakishauri kuwepo kwa ushindani wa makampuni katika masoko ya pamba ili kuimarisha uwazi na nidhamu kwa viongozi wa vyama vya ushirika.
Kupitia mpango huu wa TEHAMA na mafunzo, SHIRECU inalenga kuujenga upya ushirika wa Shinyanga unaoendeshwa kwa uwazi, ufanisi na mifumo ya kisasa ya kidijitali.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro ( wa pili kulia ) akikata utepe wakati akikabidhi Kompyuta kwa AMCOS zilizotolewa na SHIRECU
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akikabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akikabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akikabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akikabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akikabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50 

Sehemu ya Computer zilizotolewa
Sehemu ya Computer zilizotolewa
Sehemu ya Computer zilizotolewa
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kuhusu TEHAMA na uendeshaji wa ushirika na kukabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)

Mrajis Msaidizi wa Ushirika Mkoa wa Shinyanga, Ibrahim Kakozi akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu kuhusu TEHAMA na uendeshaji wa ushirika na makabidhiano ya kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)

Meneja Mkuu wa SHIRECU, Alpha Makasi akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu kuhusu TEHAMA na uendeshaji wa ushirika na makabidhiano ya kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)

Mwenyekiti wa Bodi ya SHIRECU, Naomi Mayega Chaba akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu kuhusu TEHAMA na uendeshaji wa ushirika na makabidhiano ya kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)

0 Comments