Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Arusha, wametembelea vivutio vya utalii katika Hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti sambamba na kupata mafunzo ya namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo mahali pa kazi.
Akizungumza na watumishi, Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha Mhandisi Nicholas Francis amesema hiyo ni katika kutekeleza moja ya malengo ya Taasisi hiyo lengo (A) linalohusu jinsi ya kukabiliana na HIV/AIDS, magonjwa yasiyoambukiza, ikiwa ni hatua ya kuboresha ustawi wao na kuboresha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao wawapo kazini.
Semina hiyo ililenga kuwaeleza hali halisi ilivyo ya maambukizi, njia ya kujikinga, umuhimu wa kupima kwa hiari na kwa usiri na kuondoa ile dhana za maambukizi zinazoathiri juhudi za kukabiliana na kudhibiti na kuenea kwa maambukizi ya VVU.
Aidha, washiriki walikumbushwa kuzingatia maadili, kujilinda na kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya VVU katika maisha yao ya kila siku.
Vile vile Mhandisi Nicholas aliwataka washiriki hao kuchukua tahadhari na kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara jambo ambalo litawasaidia kutambua afya zao, vile vile itawaepushia msongo wa mawazo.















0 Comments