Mamlaka ya Mapato tanzania (TRA) yaibuka Mshindi wa Kwanza wa jumla kwenye uandaaji wa hesabu za kifedha zinazozingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS). Tuzo hizo zimetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) tarehe 4 Desemba, 2025 jijini Dar es Salaam.
Vilevile, TRA imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Taasisi za Serikali (Government Agency Categories) kwenye tuzo hizo.
Aidha, tuzo hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb.) ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha katika ufungaji wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo.
Aidha, katika hafla hiyo jumla ya taasisi 86 za Umma na binafsi mbalimbali zimeshiriki katika kujipima ubora wa kuwasilisha taarifa za fedha kwa mwaka 2024.
0 Comments