
Na Oscar Assenga,TANGA
KLABU Kongwe ya Mpira wa Miguu nchini African Sports wamekabidhiwa basi jipya na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Rajabu ili kuwawezesha katika harakati zao za kupambana kurejea Ligi kuu soka Tanzania Bara
Akizungumza wakati wa akikabidhi basi hilo Abdurhaman amesema ana dhamira ya dhati kurejesha timu ya mpira wa miguu, African Spots ya jijini humo ili kurejesha heshima ya timu hiyo kongwe pamoja na Daby ya Tanga iliyokuwa na upinzani mkubwa hapa nchini.


Alisema timu hiyo imekuwa ikisuasua kupanda daraja kwa muda mrefu kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo basi la kuwasafirisha wachezaji pamoja na benchi la ufundi hivyo uwepo wa basi hilo utasaidia kuwawezesha kuondokana nazo

Aliyasema hayo Januari 24 mwaka huu katika hafla ya kuukabidhi uongozi wa timu hiyo gari Jipya aina ya TATA lililogarimu takribani shilingi Milioni 170, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Klabu hiyo barabara 12 Jijini Tanga .

Rajabu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC) alisema kwamba kurudi kwa timu hiyo kongwe hapa nchini ambayo ilianzishwa mwaka 1936 kutarejesha heshima ya Mkoa wa Tanga kutokana na kwamba bila African Spots hakuna Coastal Union inayochangiwa na utani wa jadi timu hizo kama ilivyokuwa Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam.

Mbali ya kununua basi na kukabidhi, Mwenyekiti ameahidi kusaidia timu hiyo na kuiinua hadi kufikia kucheza ligi kuu ambapo ataipambania na kujenga Jengo la Ofisi la Gorofa tatu ikiwa ni pamoja na kununua gari kubwa zaidi wakati gari iliyokabidhiwa kubaki kuwa ya kuwapeleka wachezaji mazoezini.


Sambamba na kukabidhi gari hilo mwenyekiti huyo pia alitoa kiasi cha shilingi Milioni 30 na kukabidhi kwa uongozi wa timu ya Coastal Union kwa ajili ya kutatua changamoto kadhaa zinazowakabili.


Awali akizungumza katika Halfa hiyo Rais wa TFF Walles Karia aliwasihi wanachama kushirikiana na vionhozi ili kufanya maamuzi pamoja na kujitokeza uwanjani pindi timu zitakapokuwq zancheza kwani ndio jambo sahihi la kuvuta wawekezaji.

Lakini pia aliwasihi viwanja vya michezo vilivyopo Myanjani Technically Center, "kile kituo kipo na kinafanya vizuri sana lakini kinanufaisha vijana walioko nje ya Tanga, niwasiji kwamba mpeleke vijana pale ili timu zetu zipate wachezaji bora" alisema Karia.

Katika hafla hiyo alikuwepo Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) ambaye alisisitiza suala la wanachama kushirikiana na vionhozi wa timu hiyo na kuchangia kipato kwenye timu matokeo yataonekana.

"Kama tutakuwa na timu mbili (2) zinazoenda ligi kuu, hata uchumi wa Tanga utaimarika kupitia michezo, tuchangie timu kwa kwenda uwanjani na hata kununua jezi, kwa kufanya hivyo kutaimarisha timu zetu na wachezaji kuwa na ari uwanjani" alisema.
Katika kuinua timu hizo Naibu Waziri Mwana FA alitoa kiasi cha shilingi Milioni 10 ambapo kila timu imekabidhiwa kwa vionhozi wa timu zote mbili kiasi cha shilingi Milioni 5.

Rais Karia amewahakikishia Watanzania kwamba timu ya African Spots ikismama imara kama awali na Coastal Union ndiyo timu pekee ambazo zina uwezo wa kusimamishana na Simba na Yanga na siyo timu nyingine.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi, Dk. Batilda Buriani aliwataka vionhozi wa timu za mipira na wanamichezo wote kutumia fursa ambazo zipo mkoani humo katika kuimarisha timu na kuleta manufaa katika Mkoa.
"Mradi wa Bomba la mafuta nao una fursa katika michezo, kule Uganda wamesaidia kujenga uwanja wa mpira, na hata timu yetu ya Coastal Union imeshapeleka maombi yake tunasubiri utekelezaji mwengine uendelee"
0 Comments