MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amesema, TET imejipanga kuhakikisha shule zote za Serikali zinafikiwa na vitabu kabla hazijafunguliwa.
Dkt. Komba ameyasema hayo leo Januari 10, 2026 alipotembelea ghara la TET la kuhifadhia vitabu vya kiada lililopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Amesema, tayari Serikali imechapa vitabu ya madarasa yote yanayotekeleza Mtaala ulioboreshwa na vitabu vya kujazia kwa madarasa yaliyoanza kutekeleza Mtaala ulioboreshwa mwaka 2023, pamoja na vitabu vya madarasa yanayoelekea kukamilisha Mtaala wa zamani.
"Mwaka huu wa fedha Serikali imechapa vitabu ya madarasa yote yanayotekeleza Mtaala ulioboreshwa, huku akisisitiza TET imechapa vitabu vya kujazia kwa madarasa yaliyoanza kutekeleza Mtaala ulioboreshwa, pamoja na vitabu vya madarasa yanayoelekea kukamilisha Mtaala wa zamani." Amesema Dkt. Komba.
Aidha, Dkt Komba amesema jumla ya nakala 18,628 ambazo zimejumuhisha Elimu ya Awali, Elimu ya msingi darasa la tano mpaka mpaka la saba, kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na kidato cha tano mpaka cha sita.
Ameendelea kusema, vitabu hivyo vinavyosambazwa kwa uwiano wa kitabu kimoja, mwanafunzi mmoja na uwiano wa kitabu kimoja wanafunzi watatu.
Pamoja nanhayo Dkt. Komba ameishukuru Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia TET fedha za kutosha kuendelea kuchapa vitabu na kuvisambaza katika halmashauri zote nchini.
Pia, Dkt. Komba ametoa wito kwa walimu kuvitunza vitabu hivyo na kuvitumia kwa usahihi ili kuhakikisha vinaleta tija kwa maendeleo ya elimu nchini.












0 Comments