
Hayo yamejiri Leo Jumatatu 26 Januari 2026 kwenye tukio la kuwapongeza Waalimu wa Shule ya Msingi Nanditi iliyopo Kata ya Chikunja wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Akizungumza kwenye tukio hilo Afisa Tarafa Lisekese Emmanuel Shilatu ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye tukio hilo la kuwaita Waalimu na kupongeza kwa ufaulishaji kwa asilmia 100 Wanafunzi wote.
"Nimeona niwaite niwapongeze kwa kazi nzuri ya ufaulishaji na pia iwe Chachu muendelee kufanya vizuri na kwa wengineo pia nao wafanye vizuri zaidi. Kiukweli Waalimu na Wanafunzi mmetutoa kimasomaso kwa matokeo mazuri kwa Mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba na Darasa la Nne. Kwa mfano kwa Darasa la 7 mmefaulisha Wanafunzi wote. Haijawi tokea tangu Dunia iumbwe kwa Shule yenu, hongereni sana", alisema Shilatu.
Akizungumza kwa niaba ya Wazazi Mwanaharusi Miliani ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule amewapongeza Waalimu kwa kusimamia vyema Taaluma hali inayoleta matokeo mazuri ya Watoto wetu kufaulu sana.
Pia Shilatu alipata fursa ya kuongea na Wanafunzi Darasa la 7, kukagua hali ya uripoti Wanafunzi na kujiridhisha juu ya upatikanaji wa Chakula Shuleni ambapo ameona Wanafunzi wote wakipata Chakula Shuleni.



0 Comments