SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Magharibi limefanikiwa kusajili majengo zaidi ya 2,100 yanayotumika kuhifadhi bidhaa za chakula na vipodozi katika jitihada za kuhakikisha bidhaa hizo zinahifadhiwa katika mazingira salama na kuendelea kulinda ubora wake mara baada ya kuzalishwa.
Ameyasema hayo meyasema hayo Meneja wa TBS Kanda ya Magharibi, Bw. Hamisi Seleleko wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Shirika hilo katika sekta ya viwanda ndani ya kanda hiyo.
Amesema kuwa hadi sasa TBS Kanda ya Magharibi pia imefanikiwa kutoa leseni 129 kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali katika kanda hiyo, ambapo kati ya leseni hizo 99 zimetolewa kwa wajasiriamali wadogo.
Aidha, ameeleza kuwa mahusiano mazuri kati ya TBS na Tawala za Mikoa, Wilaya pamoja na Halmashauri yamechangia kwa kiasi kikubwa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Amesema ushirikiano huo umewezesha utekelezaji wa makubaliano ya kuhudumia wananchi kwa pamoja, hali iliyosaidia kuhakikisha bidhaa nyingi zinazopatikana sokoni zinakidhi matakwa ya viwango vinavyotakiwa.



0 Comments