Ticker

6/recent/ticker-posts

BODI YA NEEC YARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EACOP

Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) pamoja na Menejimenti ya NEEC, tarehe 23 Aprili 2026 walifanya ziara maalum ya kutembelea mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika maeneo ya Ntondo mkoani Singida na Sojo mkoani Tabora.

Ikiwa ni muendelezo wa Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati, pamoja na kujifunza namna unavyochangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo husika.

Wajumbe wa bodi pamoja na menejimenti walipata fursa ya kutembelea maeneo ya ujenzi, kuzungumza na wataalamu wa mradi, na kupata maelezo ya kina kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa.

Katika eneo la Ntondo, mkoani Singida, ujumbe huo ulipokelewa na viongozi wa mradi waliowapatia taarifa juu ya maendeleo ya kazi, ikiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu na hatua za kuhakikisha usalama wa mazingira.

Wajumbe walielezwa pia kuhusu fursa za ajira kwa wananchi wa maeneo hayo na namna mradi unavyoshirikiana na jamii zinazouzunguka.

Baada ya ziara ya Singida, Wajumbe na menejimenti waliendelea na ziara katika eneo la Sojo, mkoani Tabora, ambapo walishuhudia hatua nyingine za utekelezaji wa mradi huo.

Walipata maelezo kuhusu teknolojia inayotumika katika ujenzi wa bomba hilo pamoja na mikakati ya kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa shukrani kwa waandaaji wa mradi wa EACOP kwa ushirikiano waliouonyesha, huku wajumbe wa bodi na menejimenti wakiahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo ya Taifa kupitia majukumu yao mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments