****
Na Mwandishi Wetu
Katika ulimwengu wa mahusiano ya kisasa, wengi wanakubaliana na jambo moja: dating si burudani tena—imekuwa kama kazi ya muda wote isiyo na mkataba wala masharti ya wazi.
Asubuhi unapambana na majukumu ya kikazi, jioni unapambana na hisia. Leo unapokea ujumbe wa “good morning babe,” kesho unajikuta umeachwa kwenye *blue ticks* kana kwamba uliwasilisha ombi la kazi lisilopata majibu. Hakuna mrejesho, hakuna maelezo—hata ile heshima ya “seen” haipo.
Hali hii imewaacha wengi wakijiuliza: tatizo liko wapi? Kadri mtu anavyojaribu kutafuta majibu, ndivyo uchovu wa kihisia unavyoongezeka.
Ukweli unabaki kuwa mahusiano si jambo jepesi. Na consistency—kile kitendo cha kuwa thabiti—kimekuwa kama bidhaa adimu. Watu hubadilika, hisia hubadilika, na mara nyingi kinachobaki ni mkanganyiko pamoja na maumivu yasiyoelezeka kirahisi.
Hata hivyo, katikati ya hali hiyo, kuna vitu vidogo vinavyoweza kutoa nafuu. Mfano ni utulivu wa jioni ya baridi baada ya siku ndefu, au ladha ya kwanza ya kinywaji kilichotengenezwa kwa ustadi.
Hapo ndipo bidhaa kama Gordon’s Premix Cocktail inaonekana kuleta tofauti. Kwa watumiaji wake, kinywaji hiki kinatoa uzoefu ulio thabiti—ladha ile ile kila wakati, bila kubahatisha. Hakuna maswali ya “leo itakuwaje?” wala mshangao usiotarajiwa.
Tofauti na baadhi ya mahusiano ya binadamu yenye *mixed signals*, hapa hakuna mkanganyiko. Baada ya siku ndefu ya barua pepe zisizoisha na jumbe zisizojibiwa, wengi wanatafuta kitu kisichohitaji kufikiria sana—kitu kinachofanya kazi kama kilivyoahidiwa.
Hakuna kusubiri tonic iongezwe. Hakuna visingizio. Unachofungua, ndicho unachopata.
Na pengine hapo ndipo somo linapopatikana, hasa katika msimu huu wa baridi na mvua. Consistency si kelele wala ahadi nyingi zisizotekelezwa. Ni ule utulivu wa kujua, hata bila kuuliza, kwamba mambo yako sawa.
Wakati mwingine, maisha na mahusiano yanaweza kuwa magumu kuliko inavyopaswa. Lakini si kila kitu kinahitaji juhudi kubwa kiasi hicho. Vingine vinafanya kazi kwa urahisi—kama vile cocktail iliyo tayari kunyweka.
**Mwisho.**

0 Comments