Ticker

6/recent/ticker-posts

Bondia Mashuhuri Kutoka Marekani Atua Kufanya “Royal Tour” Tanzania

Bondia mashuhuri kutoka Marekani mwenye rekodi ya kushika mikanda yote minne ya dunia katika uzito wake ukiwemo wa welterweight, Terence “Bud” Crawford, ametua nchini Tanzania leo Mei 24, 2026, kuanza “Royal Tour.”

Bondia huyo ambaye amefika kwa mwaliko wa Wizara ya Maliasili na Utalii, akiwa nchini, atatembelea Serengeti, Ngorongoro, Tarangire na Zanzibar.

“Nipo hapa kujionea uzuri wa Afrika na uzuri wa nchi hii Tanzania,” alisema Terence mara baada ya kutua Dar es Salaam.

Crawford anayetajwa kuwa miongoni mwa mabondia watatu pekee duniani pamoja na Man Pacquiao na Floyd Mayweather kuweza kuchukua mikanda minne ya dunia kwa wakati mmoja katika uzito wao, katika maisha yake ya ndondi za kimataifa hajawahi kupigwa akiwa na rekodi ya 42-0 huku akicheza pambano lake kali zaidi dhidi ya Mmexico Canelo Alvarez Septemba mwaka jana 2026 na kukosa kabisa mpinzani.

Akiwa nchini atapata pia fursa ya kufanya utalii wa michezo kwa kufundisha mbinu za kimataifa kwa mabondia wa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments