Ticker

6/recent/ticker-posts

KAHAMA JOGGING WATINGA BABATI KUHAMASISHA UTALII

Na Kijukuu Cha Bibi

Klabu ya mazoezi iliyopo manispaa ya Kahama mkoani Shinyanya ya Kahama Jogging Club leo wamefanya mazoezi ya viungo katika wilaya ya Babati mkoani Manyara na kutembelea hifadhi ya taifa ya tarangire kwa lengo la kutangaza utalii wa nchi.

Kahama jogging wamefanya ziara hiyo kufuatia mwaliko wa klabu rafiki ya Tanzanite jogging ya wilayani humo.

Kahama jogging ambao wamesafiri umbali wa kilometa 490 wameshiriki mazoezi ya pamoja ya mbio za polepole (Jogging) umbali kilometa kumi na kufanya mazoezi ya viungo (aerobic) katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo Mwenyekiti wa Kahama Jogging Abdallah Mmagane amesema kuwa ujio wao katika wilaya ya babati umelenga kufanya mazoezi na kutumia mazoezi kutangaza utalii wa Tanzania.

"Tumekuja babati kufutia mwaliko wa ndugu zetu wa Tanzanite Joggingna ujio wetu umelenga kufanya mazoezi pamoja na kutembelea hifadhi ya taifa Tarangire kwa lengo la kutangaza utalii wa nchi yetu" Amesema Mmagane.

Katika hatua nyingine Mmagane amewashukuru uongozi na wanachama wa Tanzanite jogging kwa ukarimu wao na kwamba wataendelea kudumisha urafiki uliopo kati yao na kutoa wito kwa watanzia kutembelea hifadhi za taifa zilizopo nchini kwani gharama zake ni nafuu na watanufaika na uwepo wa vivutio vingi vilivyopo hasa wanyama,ndege na miti ya asili.

"Tuwashukuru sana wenzetu wa Tanzanite jogging kwa ukarimu wao,wamekuwa ni marafiki wema sana kwetu na sisi tunawahaidi kuendelea kudumisha urafiki huu wa kimichezo,pia nitoe rai kwa watanzania wajitokeze kutembelea hifadhi za taifa kwani hakuna gharama kubwa kwa watanzania na watanufaika sana na utalii ulipo nchini mwao kama wanyama,ndege na mimea" Ameongeza Mmagane.

Naye mwenyekiti wa Tanzanite jogging Frederick Lugesha ambaye ni afisa wa NIDA Mkoa wa Manyara amesema kuwa michezo inaleta undugu na kujenga afya na kwamba walichofanya Kahama jogging ni jambo la busara kusafiri umbali mrefu na kuja kushiriki pamoja Katika michezo na kutoa wito kwa wananchi wa mkoa wa manyara hasa wilaya ya Babati kujiunga katika vikundi vya michezo ili kuweka mwili safi na kuondoka na magonjwa kama presha na kisukari na kuondoa msongo wa mawazo.

"Niwakaribishe sana ndugu zetu wa Kahama Jogging kwakweli huu ni upendo mkubwa wamefanya kwetu,niwaombe wana Manyara hasa wilaya yetu ya Babati wananchi wajitokeze kuungana nasi kufanya mazoezi ili kuondokana na magonjwa nyemelezi kama presha na kisukari pia kuondoa msongo wa mawazo" Amesema Lugesha.

Klabu ya Kahama jogging ilianzishwa julai 2021 ikiwa na jumla ya wanachama 120 kwa lengo la kufanya mazoezi na kushiriki katika matendo ya hisani kama kuchagia damu,kutembelea watoto yatima na kusaidia wasiojiweza.

Post a Comment

0 Comments