Ticker

6/recent/ticker-posts

Kikwete: Rais Samia apeleka 'kicheko' kwa watumishi wa umma

Na Mwandishi Wetu 

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa umma kufurahia utumishi wao na kupeleka furaha kwa wananchi.

Amezungumza hayo hivi karibuni mjini Arusha wakati wa kikao kazi cha maofisa tawala na rasilimali watu  huku akiwakumbusha kutekeleza wajibu wao na kuleta furaha kwa watumishi wa umma ili nao wapeleke furaha kwa watanzania.

"Nimeyaeleza hayo kufuatia maamuzi mbalimbali yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha maslahi ya watumishi wa umma yanaboreshwa. 

"...Uamuzi wa hivi karibuni wa serikali kupandisha madaraja watumishi 219,042 ni hatua ya kihistoria katika kuimarisha utumishi wa umma nchini Tanzani. Hatua hii ambayo imepata ridhaa ya Rais Samia Suluhu Hassan na ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma kwa zaidi ya asilimia 35..1 ni ishara tosha ya furaha kwa watumishi.

"Pia kuna ongezeko la kima cha chini sekta binafsi kwa zaidi ya asilimia 33.4 ambapo sekta mbalimbali zinakwenda athiriwa na maboresho haya ikiwemo afya, elimu, kilimo, mawasiliano, usafirishaji, nishati, viwanda, biashara, hoteli, michezo, uvuvi, madini na utamaduni," alisema Waziri Kikwete.

Alibainisha kwamba matokeo haya kitakwimu ni kasi ya mageuzi ya kiutumishi chini ya Rais Samia na kuakisi uongozi wa kimkakati unaoweka mbele ustawi wa watumishi na ufanisi wa taasisi za umma.

Post a Comment

0 Comments