Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Mhe. Ntuli Mwakahesya, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa PSSSF Mkoa wa Shinyanga, Nila Magambo alipotembelea banda la PSSSF katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia “Mama Samia Legal Aid” Awamu ya Pili inayofanyika katika viwanja vya Zimamoto Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Mfawidhi wa PSSSF Mkoa wa Shinyanga, Nila Magambo (kushoto), akimkabidhi zawadi Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Mhe. Ntuli Mwakahesya, alipotembelea banda la PSSSF katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia “Mama Samia Legal Aid” Awamu ya Pili inayofanyika katika viwanja vya Zimamoto Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog.
***
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Mhe. Ntuli Mwakahesya, amepongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika matumizi ya mifumo ya kidigitali inayorahisisha utoaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu.
Mhe. Jaji Mwakahesya amesema hayo Mei 8,2026 alipotembelea banda la PSSSF katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia “Mama Samia Legal Aid” Awamu ya Pili, inayofanyika katika viwanja vya Zimamoto, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuanzia Mei 6 hadi 20, 2026.
Akiwa katika banda hilo, Mhe. Jaji Mwakahesya amejionea namna mifumo ya kidigitali ya PSSSF inavyopunguza urasimu, kurahisisha upatikanaji wa huduma na kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi.
Amesema hatua hiyo inasaidia kupunguza migogoro na kurahisisha utatuzi wa changamoto mbalimbali za kisheria zinazohusiana na mafao na michango ya wanachama.
Aidha, amesisitiza kuwa matumizi ya teknolojia ndani ya PSSSF ni nyenzo muhimu katika kuwahudumia wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria, kwani yanasaidia kuongeza uwazi wa taarifa, kuimarisha uaminifu kwa wanachama na kuhakikisha haki zao zinapatikana kwa wakati.
“Matumizi ya mifumo hii ya kidigitali yanasaidia kupunguza malalamiko yanayoweza kuepukika na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi,” amesema Mhe. Jaji Mwakahesya.
Kwa upande wake, Afisa Mfawidhi wa PSSSF Mkoa wa Shinyanga, Nila Magambo, amesema banda hilo linaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko huo.
Amesema huduma zinazotolewa ni pamoja na elimu kuhusu matumizi ya Mfumo wa PSSSF Portal, huduma ya PSSSF Kiganjani, ufafanuzi wa mafao mbalimbali yanayotolewa na Mfuko, pamoja na kuwawezesha wanachama kuangalia taarifa za michango yao.
Aidha, amesema PSSSF pia inatoa huduma za msaada wa kisheria ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Awamu ya Pili inayofanyika mkoani Shinyanga.
Wananchi pamoja na wastaafu wameendelea kujitokeza kwa wingi kutembelea banda hilo kwa ajili ya kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na PSSSF.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Mhe. Ntuli Mwakahesya (kulia) , akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa PSSSF Mkoa wa Shinyanga, Nila Magambo (katikati) katika banda la PSSSF.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Mhe. Ntuli Mwakahesya (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa PSSSF Mkoa wa Shinyanga, Nila Magambo (kulia) katika banda la PSSSF.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Mhe. Ntuli Mwakahesya (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa PSSSF Mkoa wa Shinyanga, Nila Magambo (kulia) katika banda la PSSSF.
Afisa Mfawidhi wa PSSSF Mkoa wa Shinyanga, Nila Magambo (kushoto), akimkabidhi zawadi Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Mhe. Ntuli Mwakahesya, alipotembelea banda la PSSSF.
Wateja wakipata huduma na elimu mbalimbali katika banda la PSSSF wakati wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia “Mama Samia Legal Aid” mjini Shinyanga.

Mwananchi akipata huduma katika banda la PSSSF wakati wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia “Mama Samia Legal Aid” mjini Shinyanga.

0 Comments