Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YASHIRIKI MKUTANO WA 28 WA VIWANGO AFRIKA MASHARIKI

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki Mkutano wa 28 wa Kamati ya Viwango Afrika Mashariki (EASC) uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha kuanzia Mei 12 hadi 14, 2026, kwa lengo la kutekeleza mpango kazi wa viwango, upimaji, metrolojia na ubora wa bidhaa (SQMT).

Mkutano huo unatajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa Tanzania kwani utaimarisha biashara ndani ya nchi wanachama wa EAC, kukuza viwanda vya ndani pamoja na kuongeza ubora wa bidhaa za Tanzania katika soko la kikanda na kimataifa

Post a Comment

0 Comments