**
Dar es Salaam ilishuhudia weekend ya kipekee ya burudani, fashion, elegance na celebration baada ya Serengeti Premium Apple kuandaa mfululizo wa matukio ya kusherehekea Siku ya Mama Duniani yaliyofanyika katika maeneo ya Upper Deck, Hyatt Regency, na Maison Femme.
Wanawake mbalimbali kutoka kwenye taaluma tofauti, sekta za mitindo, ubunifu, lifestyle, media na burudani walijitokeza kwa muonekano wa kuvutia na wa kifahari kusherehekea pamoja na mama zao, marafiki, na wanawake wenzao wanaowapa hamasa kwenye maisha yao ya kila siku.
Kuanzia mitindo ya mavazi ya kuvutia, mionekano ya kipekee, na kufurahia nyakati za kipekee pamoja mpaka kufanya ‘toast’ pamoja na mama zao, weekend hiyo iligeuka kuwa celebration ya kisasa iliyochanganya mitindo, urembo, usasa na kujumuika pamoja katika mazingira ya kipekee yaliyojaa furaha na upendo.
Katika kila location, wageni walipokelewa kwa glass maridadi ya kinywaji cha Serengeti Premium Apple ambacho kimetengezwa hapa nchini na kampuni ya Serengeti Breweries Limited kabla ya kushiriki kwenye #ToastToMoms, moment maalum iliyowapa nafasi ya kuelezea sababu zao za kumsherehekea mama yao au wanawake waliowalea na kuwahamasisha maishani.
Mbali na kusherehekea Siku ya Mama Duniani, experiences hizo pia ziliendelea kuonyesha misingi ya chapa mpya ya Serengeti Premium Apple iliyotengenezwa Tanzania ikiwa na ladha ya hadhi ya kimataifa ambayo ni: ladha yake laini ya apple, yenye kuburudisha na rahisi kufurahia kunywa, kuendelea kusherehekea wanawake wa kisasa wenye kujiamini na hadhi, pamoja na kuvumbua namna mpya za kufurahia mitindo mipya na ya kisasa ya maisha kupitia nyakati tofauti zinazounganisha watu.
Kupitia mazingira ya kifahari, muziki, mitindo ya mavazi, kufurahia chakula na vinywaji, kujumuika kwa pamoja kupitia nyakati zenye hadhi ya kipekee, Serengeti Premium Apple inaendelea kujitambulisha kama kinywaji kinachowakilisha kizazi cha kisasa cha Watanzania wanaopenda fahari yao, kujumuika kwa pamoja, na kusherehekea maisha kwa namna tofauti.
Kwa wengi waliohudhuria, #ToastToMoms haikuwa tu event ya Mother’s Day, ilikuwa celebration ya womanhood, confidence, style na appreciation.










.jpg)









0 Comments