Ticker

6/recent/ticker-posts

UNESCO NA NACTVET WAZINDUA KOZI MTANDAO YA ELIMU YA STADI ZA MAISHA NA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI TVET

Tanzania imepiga hatua muhimu katika kuboresha afya na ustawi wa vijana kwa uzinduzi rasmiwa Kozi Mtandao ya Elimu ya Stadi za Maisha na Afya ya Uzazi (CSE) chini ya mradi wa“Maisha yetu, Haki Zetu, Mustakabali wetu”- (O3 Plus). 

Mradi huu unatekelezwa kupitia ushirikiano kati ya UNESCO na National Council for Technical and Vocational Education and Training (NACTVET), ikiwa ni hatua muhimu katika kuongeza upatikanaji wa elimu borana sanifu ya afya kwa wanafunzi wa vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET).

Kozi hii imeidhinishwa rasmi na NACTVET na kuunganishwa katika mfumo wake wa elimumtandao (Learning Management System), hivyo kuwawezesha wanafunzi katika vyuo saba – IFM, CBE, NIT, DIT, WIT, TPSC and KIUSO vilivyochaguliwa kuanza kuisoma katika awamuya kwanza ya utekelezaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mwakilishi Mkazi na Mkuu Wa ofisi ya UNESCO Bw. Michel Toto ilieleza kuwa mpango huu hauhusu elimu pekee, bali unalenga kuwajengea vijana uelewa, kujiamini, na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya zao, mahusiano, matumizi ya fedha, na mustakabali wao.

Kwa upande wake, NACTVET ilibainisha kuwa mpango huu unaendana na viwango vya kimataifa na kitaifa na unalenga kuimarisha ustawi wa wanafunzi, usawa wa kijinsia, pamoja na mazingira salama na jumuishi ya kujifunzia. 

Aidha, ilielezwa kuwa utekelezaji wa awamu ya kwanza utatoa uzoefu na mafunzo muhimu yatakayosaidia kupanua mpango huu katika vyuo vingine zaidi nchini vilivyopo chini ya NACTVET.

Uzinduzi huu pia umeimarisha dhamira ya vyuo shiriki kusaidia utekelezaji kupitia mifumo madhubuti ikiwemo kutoa msaada utakaohitajika katika kuisoma kozi mtandao (technical support), kuwajengea uwezo waelimisha rika, na kuimarisha mifumo ya kushughulikia ukatili wa kijinsia (GBV).

Mpango huu ni sehemu ya juhudi za kitaifa za kuwawezesha vijana balehe kwa kuwapatia taarifa sahihi za kiafya na stadi muhimu za maisha. 

Wadau wote wamethibitisha upya dhamira yao ya kukuza mpango huu ili kuhakikisha kila mwanafunzi anamaliza safari yake ya masomo bila vikwazo na kufikia ndoto yake.

Post a Comment

0 Comments