Waziri wa Madini , Anthony Mavunde akiongea kwenye ufunguzi wa Jukwaa la tano la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini nchini, unaondelea jijini Mwanza.
Waziri wa Madini , Anthony Mavunde , akipata maelezo ya utekelezaji wa sheria na kanuni za Maudhui ya ndani kutoka kwa Meneja Ugavi wa Barrick, Victor Ndamgoba alipotembelea banda hilo
Mkuu wa Kitengo cha Ugavi wa Barick North Mara, Enock Otieno akizungumza kwenye mdahalo wa Jukwaa la tano la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini
Wafanyakazi wa Barrick wakiwa katika banda lao
Wafanyakazi wa Barrick wakiwa katika banda lao
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick wakisikiliza hotuba ya Waziri Mavunde kwenye jukwaa hilo
Wafanyakazi kutoka makampuni yaliyotoa udhamini mkubwa wa Jukwaa katika picha na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde na watendaji waandamizi wizara.
**
Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga imeeleza dhamira yake ya kuendelea kunufaisha watanzania wengi kupitia utekelezaji wa sera ya ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini (Local Content) kupitia manunuzi ya bidhaa za ndani,ajira na uwezeshaji wa wazawa.
Akiongea katika mdahalo wa utekelezaji sera hii katika jukwaa la tano la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini linaloendelea jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Ugavi wa Barick North Mara, Enock Otieno amesema fursa zipo nyingi katika migodi ya Barrick hivyo wanapaswa kuzichangamkia huku wakizingatia suala la kukidhi viwango vya bidhaa na huduma zinazotakiwa.
Ameongeza kwamba ni muhimu kwa watanzania kuanza kujifunza kwa kasi teknolojia ya uchimbaji wa madini na kuhakikisha bidhaa na huduma zao zinakuwa kwenye viwango vinavyokubalika na wawekezaji kwenye sekta ya madini.
“Kuna mambo makuu matatu ambayo watanzania wengi wanashidwa kufikia viwango vya utoaji huduma kwenye migodi ambayo ni gharama za kuhudumia mradi husika, ubora wa bidhaa na huduma na uwezo wa kuwa na teknolojia ya kisasa,” alisisitiza Otieno.
Amesema kwamba pamoja na serikali kupitia wizara ya madini kuweka sheria na kanuni za maudhui ya ndani kwa ajili ya kufungua milango kwa watanzania kushiriki kwenye sekta ya madini ila ni muhimu kwa watanzania kuanza kujifunza mabadiliko ya teknolojia kwenye uchimbaji wa madini ili kuendelea kukuza mnyororo wa thamani.
Amesema ni muhimu wa watanzania wazawa ambapo ni wazabuni kwenye sekta ya madini kuja na mbinu za ubunifu kwenye bidhaa na huduma wanazotoa ili kuendelea kujitangaza kwenye sekta ya madini hapa nchini.
Otieno amesisitiza kuwa pamoja na mambo mengine ni muhimu kwa watanzania kuzingatia ubora wa bidhaa na huduma wanazotoa kwa makampuni ya uchimbaji wa madini nchini.
Katika Hotuba ya ufunguzi katika Jukwaa hilo , Waziri Madini , Anthony Mavunde amesema kwamba sekta ya madini imeendelea kukua kwa kasi kubwa na kutoa mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa (GDP) , kodi na mapato mengine yasiyo ya kikodi.
“Mpaka kufikia mwisho wa mwezi wa sita mwaka huu , sekta hii ya madini imechangia kiasi cha shilingi 1.4 Trillioni kwenye mfuko mkuu wa serikali kwa mapato yasiyo ya kikodi , haya ni mapinduzi makubwa kubwa sana tumefanya kama taifa ,” amesema Mavunde.
Amesema kwamba kwa muda mrefu kilio cha watanzania ilikuwa ni jinsi ya kushiriki kwenye sekta ya madini ambapo awali shughuli zote za migodini zilikuwa zinachukuliwa na wageni lakini baada ya kutungwa kwa sheria ya maudhui ya ndani na kanuni zake watanzania wameanza kunufaika na mabadiliko hayo.
Awali Mavunde alipotembelea banda la maonesho la Barrick-Twiga ameipongeza kampuni ya Barrick-Twiga ameipongeza kwa mchango wake katika ukuzaji wa sekta ya madini nchini.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Tume ya Madini , Dkt Janet Lekashingo amesema kwamba sekta ya madini ni kichocheo cha ukuaji wa sekta ya viwanda na kupanua wigo wa mnyororo wa thamani nchini.
Ameongeza kwamba utekelezaji wa sheria , kanuni , sera na miongozo ni chachu ya maendeleo ya viwanda kwa kupunguza ajira , kipato na ukuaji wa uchumi wa nchini.







0 Comments