Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026, yakionyesha ongezeko la ufaulu ambapo asilimia 99.92 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Ally Mohamed, amesema watahiniwa 125,056 kati ya 125,320 waliopata matokeo wamefaulu kwa madaraja ya Kwanza hadi Nne. Idadi ya waliopata Daraja la Kwanza imeongezeka kutoka 61,020 mwaka 2025 hadi 67,606 mwaka 2026.
Aidha, zaidi ya asilimia 99.6 ya watahiniwa walipata madaraja ya Kwanza, Pili na Tatu, huku karibu masomo yote yakirekodi ufaulu wa zaidi ya asilimia 93. Pia, hakuna shule iliyopata wastani wa Daraja F mwaka huu.
0 Comments