Na Mwandishi wetu Bagamoyo
Wakala wa Misitu nchini (TFS) wamepokea wameanza kupokea wageni kutokana na Punguzo la Msimu huu wa sabasaba katika kutembelea vituo vyao vya utalii.
Zoezi hilo limeanza rasmi kwa kupokea Wageni wa ndani na nnje ya nchi waliotembelea Mji wa bagamoyo katika eneo la kijiji cha Kaole kilichopo wilayani Bagamoyo ili kuona na kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo magofu ya kale.
Akizungumza katika eneo la magofu ya kale Mhifadhi Veronica ameendelea kuwasihi wananchi juu ya kutembelea vivutio mbalimbali nchini akiwasisitiza kujitokeza katika safari nyingine ya Tarehe 11, kuelekea Pugu kazimzumbwi kwa utaratibu wa ofa ya sabasaba.
Aidha mmoja wa wageni wa hao amesema kuwa wamefurahi kufika katika mji wa bagamoyo na kijiji cha kaole na kujionea vyote walivyokuwa wakivisikia awali.
















0 Comments