Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Evodi Kereti,(aliyevaa kofia kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Julius Mtatiro ( wa pili kutoka kushoto aliyevaa kofia), moja ya vitanda vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM), wakati wa hafla ya SHYCOM Alumni Half Marathon 2026. Picha na Stela Paul

Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Evodi Kereti,(wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Julius Mtatiro ( wa tatu kutoka kushoto), moja ya vitanda vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM), wakati wa hafla ya SHYCOM Alumni Half Marathon 2026.
Makabidhiano yakiendelea, Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Evodi Kereti, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Julius Mtatiro, moja ya vitanda vilivyotolewa na CRDB Bank kwa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM), wakati wa SHYCOM Alumni Half Marathon 2026.
Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Evodi Kereti (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Julius Mtatiro (kushoto), moja ya vitanda vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM), wakati wa hafla ya SHYCOM Alumni Half Marathon 2026.
Na Stela Paul, Shinyanga
Benki ya CRDB imekabidhi vitanda 20 vya ghorofa mbili (double decker) vyenye uwezo wa kulaza wanafunzi 40 katika Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuishi kwa wanafunzi wa chuo hicho.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo, Septemba 26, 2026, wakati wa Mashindano ya SHYCOM Alumni Half Marathon 2026, iliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage, Manispaa ya Shinyanga.
Vitanda hivyo vimepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Julius Mtatiro, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita.
Mtatiro ameipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo ya kushirikiana na Serikali na wadau wa elimu katika kuboresha mazingira ya wanafunzi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Evodi Kereti, amesema msaada huo ni sehemu ya mchango wa benki hiyo katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na SHYCOM Alumni, katika kuboresha mazingira ya chuo hicho.
Kereti amesema Benki ya CRDB imeamua kushiriki katika mpango huo kutokana na kutambua umuhimu wa elimu na mazingira bora kwa wanafunzi, huku akiwashukuru wahitimu wa SHYCOM na wadau wengine kwa kuendelea kuwa sehemu ya wateja na wadau wa benki hiyo.
“Msaada huu ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali pamoja na SHYCOM Alumni katika kuboresha mazingira ya wanafunzi. Tunawashukuru pia SHYCOM Alumni kwa kuendelea kuwa wateja wa CRDB Bank,” amesema Kereti.
Amesema Benki ya CRDB itaendelea kuwa sehemu ya wadau wanaounga mkono SHYCOM Alumni Half Marathon, huku akiahidi kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana kwa karibu na waandaaji wa mbio hizo katika misimu ijayo.
“Benki ya CRDB itaendelea kuwa mdhamini wa SHYCOM Marathon na kuwa mdau wa karibu katika kuhakikisha shughuli hizi zinaendelea kuleta matokeo chanya kwa jamii na chuo,” amesema.















0 Comments