Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

FAMILIA ZATAKIWA KUWA NA MPANGO WA KUKABILIANA NA MAAFA







Na Mwandishi wetu, Rukwa

‎Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka familia kuwa na mpango wa kukabiliana na maafa kabla hayajatokea ili kuzijengea uwezo wa kukabiliana nayo pindi yanapotokea.

‎Ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2026 Mjini Sumbawanga kwenye Uwanja wa Nelson Mandela ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa na kusisitiza kuwa ili kuweza kukabiliana na maafa ni lazima mipango hiyo kuanza katika ngazi ya familia.


Amesema, wakati Serikali ikiendelea kukabiliana na majanga ikiwa ni pamoja na kudhibiti mianya mbalimbali ya maafa upo umuhimu mkubwa wa jamii kuanzia ngazi ya familia kuwa na mikakati ya kukabiliana na maafa kabla na baada ya kutokea.

Aidha, ‎Dkt. Nchemba amesema kuwa, maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “Ustahimilivu unaanzia nyumbani” hivyo inatukumbusha namna ambavyo jamii zimekuwa zikipitia madhira kupitia maafa mbalimbali licha ya kuwaachia makovu yasiyosahaulika.

‎Waziri mkuu huyo alifafanua kuwa mbinu za kukabiliana na maafa kulingana na mazingira inahitaji jamii husika kubeba jukumu la kuhakikisha inapewa mbinu za kisasa ikiwa ni pamoja na zile za jadi hiyo itasaidia kupunguza ukubwa wa majanga pale yanapotokea kwa maana jamii husika itakuwa imekabiliana nayo kwa kiasi kikubwa.


Ha hivyo amesema, ‎Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa iliasisiwa mwaka 1989 kama njia ya kupunguza vihatarishi vya maafa duniani ambavyo vimekuwa vikiacha huzuni kwa watu

‎


"Suala la mabadiliko ya tabia ya nchi ni moja ya visababishi vya maafa mbalimbali, jamii na Serikali kwa ujumla wanalo jukumu la kuimarisha mapambano ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kila jamii husika inauelewa mkubwa juu ya mabadiliko hayo na namna ya utatuzi wake." Amesema Mhe. Mwigulu Nchemba
‎

Pamoja na hayo Mhe. Waziri Mkuu ‎ametoa mifano mbalimbali ya maafa ambayo Watanzania wameyapitia ikiwa ni pamoja na maporomoko ya Hanang na Mbeya, Mafuriko na ajali ambazo zimewaachia Watanzania wengi na majonzi makubwa.




‎Pia Waziri Mkuu ameitumia fursa hiyo kupata taarifa ya maandalizi ya shughuli za kuzima Mwenge wa Uhuru ikiwa ni pamoja na wiki la vijana ambapo Waziri wa Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka alieleza maandalizi kwa ujumla yamefikia asilimia 100 huku wiki ya vijana imetumika vizuri katika kuwajenga vijana kuwa wajasiri na kuzitambua fursa.

Post a Comment

0 Comments