Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

TCAA NA MASHIRIKA YA NDEGE YAIMARISHA USHIRIKIANO KUBORESHA UFANISI WA HUDUMA

 

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na wawakilishi wa mashirika 13 ya ndege wamekutana mjini Kibaha katika kikao kazi chenye lengo la kuimarisha ushirikiano, kuboresha mifumo ya utoaji huduma na kuongeza ufanisi katika Sekta ya Usafiri wa Anga kupitia Mfumo wa Huduma za Usafiri wa Anga (CASP).

Akizungumza katika kikao hicho, kilichofanyika Oktoba 18, 2026 Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Dkt. Jabiri Bakari, amewahimiza waendeshaji wa mashirika ya ndege kuachana na taratibu za zamani zilizotegemea kutembelea ofisi ana kwa ana na badala yake kutumia CASP kupata huduma kwa urahisi na ufanisi zaidi.

 Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha nyaraka na taarifa zinawasilishwa kwa usahihi na kwa wakati, huku akiwataka viongozi wa mashirika hayo kusambaza maelekezo kwa wafanyakazi wao ili kurahisisha matumizi ya mfumo na kufikia malengo ya utekelezaji ndani ya muda uliokubaliwa.

Dkt. Bakari ameeleza kuwa changamoto za kiufundi zinaweza kujitokeza katika hatua za awali za matumizi ya mfumo mpya, akiwahimiza watumiaji kutoa mrejesho na kutumia dawati la msaada lililoanzishwa kwa ajili ya kupata usaidizi wanapokumbana na changamoto. 

Dawati hilo linapatikana kupitia njia mbalimbali, zikiwemo simu ya bure, WhatsApp, barua pepe na majukwaa mengine ya mtandao.

Kwa upande wao, wawakilishi wa mashirika ya ndege wamepongeza juhudi za TCAA. 

 Pia, wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu na mawasiliano ya wazi kati ya TCAA na mashirika ya ndege katika kutatua changamoto na kuboresha huduma.

Post a Comment

0 Comments