Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

TRA KUENDELEA KUWAWEZESHA WAKULIMA WA MIWA KUFANYA BIASHARA

  

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, ametembelea Kiwanda cha Sukari cha Kilombero mkoani Morogoro na kuahidi kuwawezesha wakulima wa miwa kufanya biashara zao kwa urahisi huku wakizingatia sheria za kodi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Oktoba 19, 2026, Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA itaunda timu ya wataalamu itakayochunguza mwenendo wa biashara na taarifa za wakulima wa miwa wanaouza mazao yao katika viwanda vya sukari, kwa lengo la kutafuta njia bora za kuwawezesha kuendelea na biashara zao kwa kuzingatia sheria.

Amesema timu hiyo itafanya kazi kwa siku 30, ikipitia kanzidata za viwanda vya sukari ili kubaini namna bora ya kurahisisha upatikanaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa wakulima wa miwa na kuwawezesha kutekeleza wajibu wao wa kikodi bila vikwazo visivyo vya lazima.

Aidha, Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA imejipanga kuendelea kuwezesha biashara nchini kwa kuboresha mazingira ya ulipaji kodi na kuondoa changamoto zinazoweza kuathiri shughuli za kiuchumi. 

Ameipongeza Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwa kuzingatia sheria za kodi na kuhimiza ushirikiano kati ya TRA, viwanda na wakulima kwa manufaa ya sekta ya sukari na uchumi wa taifa.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, Bw. Fakihi Fadhili, amemshukuru Kamishna Mkuu kwa ziara hiyo na jitihada za TRA za kurahisisha mazingira ya biashara. 

Amesema kiwanda hicho kinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa lengo la kuchangia upatikanaji wa sukari ya kutosha nchini, sambamba na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

Post a Comment

0 Comments