Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

WANANCHI KIGOMA WAHIMIZWA KUTOA HOJA KABLA UTHAMINI KUKAMILIKA

 

Mthamini Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rashid Mageta, akiwa na wataalamu wengine katika eneo la Mguswa, Kigoma, wakijiridhisha na taarifa za uthamani wa mali zinazohusika na Mradi wa SGR Lot 6. Ili kuhakikisha usahihi na zinazingatia hali halisi ya mali za Mwananchi.

***

KIGOMA

Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamehimizwa kutumia kikamilifu zoezi la kuhakiki taarifa za mali zao na kutoa maoni pale wanapoona kuna taarifa ambazo hazijaandikwa kwa usahihi katika mchakato wa uthamini.

Mthamini Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rashid Mageta, amesema disclosure ni sehemu muhimu ya mchakato wa uthamini inayompa mwananchi fursa ya kushirikiana na mthamini katika kuhakiki taarifa za mali yake kabla ya mchakato kukamilika.

Amesema zoezi hilo linampa mwananchi nafasi ya kuona taarifa zilizokusanywa kuhusu mali yake na kueleza endapo kuna jambo ambalo halijaakisi hali halisi, ili kuwezesha marekebisho kufanyika mapema pale hoja inapobainika kuwa na msingi.

“Disclosure ni kama kioo kati ya mthamini na mwananchi. Mwananchi anapata nafasi ya kuhakiki taarifa zake na kueleza pale anapoona kuna kosa,” amesema Mageta.

Mageta amesema utaratibu huo umewekwa kwa mujibu wa Kanuni Na. 64 za Uthamini na Usajili wa Wathamini, kwa lengo la kuhakikisha changamoto zinazoweza kujitokeza zinabainishwa na kushughulikiwa mapema.

Katika utekelezaji wa zoezi hilo mkoani Kigoma, jumla ya wananchi 886 wamepangwa kufikiwa kwa ajili ya zoezi la disclosure, ambapo hadi sasa wananchi 819, sawa na takribani asilimia 92.4, kutoka maeneo ya Masanga, Mungonya, Msufini na Butunga, wamefikiwa na kupata fursa ya kuhakiki taarifa zao za mali na fidia.

Aidha, wananchi 67, sawa na takribani asilimia 7.6, ambao bado hawajafika kuhakiki taarifa zao, wamehimizwa kutumia fursa hiyo na kufika katika maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya disclosure ili kuhakiki taarifa zao na kutoa hoja mapema.

Amesema ushiriki wa wananchi katika zoezi hilo ni muhimu kwa kuwa unawawezesha kuhakiki taarifa zinazohusu mali zao na kutoa maoni au hoja kabla ya mchakato wa uthamini kukamilika.

Ametoa wito kwa wananchi ambao bado hawajafika katika maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya disclosure kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kuhakiki taarifa zao na kutoa hoja mapema badala ya kusubiri mchakato wa uthamini kukamilika.

Amesisitiza kuwa ushiriki wa wananchi katika disclosure unasaidia kuhakikisha taarifa za mali na fidia zinaandaliwa kwa kuzingatia hali halisi ya mali husika pamoja na taratibu za kitaalamu za uthamini.

Post a Comment

0 Comments