Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB YAJA NA MKAKATI MAALUMU KUWASAIDIA WASTAAFU


 Meneja Mahusiano kwa Wateja wa makundi Maalumu CRDB, Bi.Optune Kaihula akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam katika Semina ya Wastaafu Watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).


*****************************


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


Benki ya CRDB kama mdau wa Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na wananchi wote kwa ujumla wameshiriki semina ya Wastaafu Watarajiwa iliyoandaliwa na mfuko huo ili kuweza kutoa huduma na elimu kuhusiana na fedha pamoja na uwekezaji.

Akizungumza katika Semina hiyo Meneja Mahusiano kwa Wateja wa makundi Maalumu CRDB, Bi.Optune Kaihula amesema wamekuja sokoni na akaunti ya wastaafu ambayo ni akaunti mahususi kwaajili ya kufikisha pensheni zao na viunua mkongo vyao.

Amesema wamewaletea wastaafu akaunti ya kuwekeza ambayo wanaweza kuwekeza fedha zao ndani ya miaka mitatu lakini ndani ya miaka hiyo kila mwezi wanaweza kupokea faida.

"Hili kuwajengea uwezo pale ambapo alikuwa anapokea mshahara na amestaafu mshahara haupo tena kwahiyo kwa kupokea faida za fedha zake ambazo amewekeza CRDB tunamuwekea ile hali ya kupata mshahara huku anapata faida huku anapata pensheni yake kila mwezi". Amesema 

Aidha amesema kuwa wameweka mkopo ambao ni wamuda mfupi na wamuda mrefu.Mkopo wa muda mfupi mteja anaweza kukopa pensheni advance ndani ya mwezi mmoja na pensheni yake ikipita italipa ule mkopo na ataweza kukopa tena.

Pamoja na hayo amesema wameweka pia mkopo wa muda mrefu ambao unaanzia mwaka mmoja mpaka miaka saba na unaweza kukopa Milioni moja hadi Milioni 100 na mkopo huo una bima, lolote likitokea insuarance itaweza kulipa mkopo wake wote na wataweza kutooa mkono wa pole kiasi cha Milioni moja kwa familia iliyobaki.


Post a Comment

0 Comments