Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA SIASA SINGIDA YARIDHISHWA NA UTEKELEZWAJI WA MIRADI WILAYA YA SINGIDA NA MANISPAA.




Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, wakikagua ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida leo.



Mjumbe wa Kamati ya siasa Mkoa wa Singida, Martin Lissu (kulia) akielekeza jambo wakati kamati hiyo ilipokuwa ikikagua maabara ya Shule ya Sekondari ya Merya.
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Sekondari ya Manguapyughu iliyopo Kata ya Unyambwa
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua vyoo vya Shule ya Sekondari ya Manguapyughu iliyopo Kata ya Unyambwa
Ukaguzi wa uboreshaji wa miundombinu ya huduma za maji eneo la Mungumaji ukifanyika.




Ukaguzi wa ukarabati wa Barabara ya Majengo hadi Unyamikumbi ambayo imegharimu Sh.159 Milioni ukifanyika.
Ukaguzi wa Kiwanda cha Ushonaji wa nguo cha Kikundi cha Wanawake (WAVUMA) cha Ilongero ukifanyika.



Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ilongero ukiendelea.

Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya Ilongero.


Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, wakikagua chumba cha maabara ya Shule ya Sekondari ya Merya.



Wajumbe hao wakikagua ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ya Sekondari Maghojoa.




Na Dotto Mwaibale, Singida.




KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida imekagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Singida Manispaa na kuridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti jana wakati kamati hiyo ikikagua miradi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa , Alhaji Juma Kilimba alisema ameridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo katika halmashauri hizo.

"Kwa kweli tunawapongeza kwa kuitendea haki miradi hii ambayo Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza," alisema Kilimba.

Kilimba alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii badala ya kuisubiri Serikali.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.

Aliwaomba wananchi kila ilipotekelezwa miradi hiyo kuitunza ili iendelee kuwa na manufaa kwao.

Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo waliwapongeza wakuu wa shule na viongozi waliosimamia fedha za kutekeleza miradi hiyo kwa kuwa waaminifu na kufanikisha miradi hiyo.

Baadhi ya miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo katika Wilaya ya Singida ni ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ujenzi wa wodi tatu za Hospitali ya Wilaya Ilongero, ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Nyeri, ujenzi wa bweni moja na matundu 12 ya vyoo Shule ya Sekondari Maghojoa, ujenzi wa madarasa matatu na ofisi moja Shule ya Msingi Msange na ukamilishaji wa maabara Shule ya Sekondari Merya.

Katika Manispaa ya Singida miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa jengo la mama na mtoto Zahanati ya Mwankoko, ukamilishaji wa maabara Shule ya Sekondari Mtipa, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu saba ya vyoo Shule ya sekondari ya Manguapyughu Iliyopo Kata ya Unyambwa, uboreshaji wa miundombinu ya huduma za maji eneo la Mungumaji, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Sekondari Mwenge na ukarabati wa barabara ya Majengo hadi Unyamikumbi ambayo imegharimu Sh.159 Milioni.

Ziara hiyo iliwahusisha viongozi na wataalamu mbalimbali wa wilaya hizo pamoja na Mkuu wa Wilaya hizo Mhandisi Paskas Muragili.

Kesho kamati hiyo itafanya ziara ya namna hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na Itigi.

Post a Comment

0 Comments