Ticker

6/recent/ticker-posts

MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA AJIRA ZA JESHI LA POLISI TANZANIA

 

 

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camilius Wambura amewatangazia vijana walioomba kuajiriwa na Jeshi la Polisi usaili wao utafanyika kuanzia Januari 23, 2023 hadi Februari 3, 2023 nchini kote.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Januari 17, 2023 na IGP Wambura, waombaji wenye elimu ya kidato cha nne waliowasilisha maombi yao kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa usaili wao utafanyika kwenye mikoa waliyowasilisha maombi yao.


Aidha, waombaji wa Zanzibar wenye elimu ya shahada, stashahada ya juu, stashahada na astashahada usaili wao utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na waombaji wenye elimu ya kidato cha nne usaili wao utafanyika kwenye mikoa waliyowasilisha maombi yao.

"Waombaji wa Tanzania Bara wenye elimu ya shahada, stashahada ya juu, stashahada na astashahada ambao walituma maombi yao kwa njia ya mtandao, usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam katika Vikosi vya Polisi vilivyoainishwa kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili.


"Aidha usaili huo utafanyika kwa makundi mawili (2), kundi la kwanza litaanza Januari 23,2023 hadi Januari 27,2023 na kundi la pili litaanza Januari 30, 2023 hadi Februari 3,2023.


"Kila mmoja atatakiwa kufika na vyeti halisi vya taaluma (academic certificates), cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa (NIDA) au namba ya NIDA na cheti cha JKT au Barua ya Uthibitisho toka kwa Mkuu wa Kambi (Kwa vijana walio kwenye makambi ya JKT/JKU),"amefafanua IJP Wambura kupitia taarifa hiyo.Orodha ya vijana waliochaguliwa kufanya usaili jijini Dar es salaam hii hapa chini;


Post a Comment

0 Comments