Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKUMBUSHO YA TAIFA YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI


Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa akiwafafanulia jambo Wahariri wa vyombo vya habari kwenye mkutano wake na Wahariri hao (Hawapo pichani), Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma Makumbusho ya Taifa Bi Joyce Mkinga.

Mhariri wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw Amin Mgeni akishauri jambo kwenye mkutano wa wahariri na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Tanzania

Mhariri wa Izaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW) Bi Hawa Bihoga, akishauri jambo kwenye mkutano wa wahariri na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Tanzania

Picha ya pamoja kati ya uongozi wa Makumbusho ya Taifa na baadhi ya Wahariri wa vyombo vya Habari nchini.

****************************

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga, amekutana na Wahariri wa vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi na kuwaomba kushirikiana na taasisi yake katika kutangaza urithi wa asili na utamaduni wa nchi ya Tanzania.

Katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Wahariri vya vyombo mbalimbali vya habari, Dkt Lwoga aliwafahamisha wahariri hao kuhusu Makumbusho ya Taifa, shughuli zake za msingi, programu na huduma mbalimbali pamoja na mikakati ya taasisi hiyo katika kuboresha huduma zake za uhifadhi na uendelezaji wa mikusanyo ya kimakumbusho na ya Malikale.

Dkt Lwoga alisema kuwa, vyombo vya habari vinanafasi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya utajiri wa urithi wa utamaduni na Malikale uliohifadhiwa kwenye makumbusho hizo zilizopo Dar es Salaam, Arusha, Butiama, Songea pamoja na vituo zaidi ya 90 vya Malikale kote nchini ili jamii iweze kunufaika navyo kielimu na kiburudani.

Licha ya kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa hatua mbalimbali inazozichukuwa za kuboresha huduma zake na kuwa karibu na vyombo vya habari, Mhariri wa Clouds Media Bi Joyce Shebe aliishauri Taasisi kuvishirikisha vyombo vya habari katika program mbalimbali zinazoendeshwa na Makumbusho ya Taifa.

“Kwa kweli nilipo pokea mwaliko wa kuudhuria kikao hiki nilishangaa kidogo, kisha nikasema sasa Makumbusho imebadilika maana sikuwahi kuwaza kama mtatuita ili tufahamu zaidi kutoka kwenu na ninyi mpokee mawazo yetu kuhusu kuboresha mikakati yenu ya kufikisha taarifa kwa jamii, tunapo pata elimu hizi tunakuwa na uwelewa mpana kuhusu nini mnafanya hapa, hongereni sana” Alisema Joyce Shebe.

Naye Mhariri kutoka Shirika la Utangazaji nchini (TBC) Bw. Amini Mgeni, ameishauri Makumbusho ya Taifa kubuni program nyingi za matamasha yatakayohamasisha utalii wa ndani hasa eneo la Kilwa lenye vivutio vingi vya Malikale na asilia kama vile fukwe zilizo beba urithi wa kihistoria kabla ya Uhuru na kipindi cha harakati za kutafuta Uhuru wa nchi yetu.

Akiwasilisha mada kuhusu Makumbusho ya Taifa na Mkakati wa Kujitangaza, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma, Bi Joyce Mkinga amewaeleza wahariri hao kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu na vyombo vya habari katika kutangaza mikusanyo, malikale na huduma za Taasisi hiyo.

“Mpango wetu wa mwaka 2021/2022 ni kuandaa Mkakati wa Masoko na Mawasiliano, Kuboresha huduma zetu, kuongeza bajeti ya utangazaji kwa kutafuta wafadhili, kuandaa semina za mara kwa mara na ziara za Wahariri na Waandishi wa habari kutembelea vivutio vyetu nchini na kuboresha mahusiano na wadau” Aliongeza Bi Mkinga

Bi Mkinga aliwashukuru wahariri hao, kwa kuudhuria kikao hicho cha kuimariha mahusiano na kuwaomba waendelee kuwa karibu na Makumbusho ya Taifa ili kujipatia Maudhui ya urithi wa asili na kiutamaduni kwa aliji ya wasomaji, wasikilizaji na waangaliaji wa vyombo vyao vya habari.

Post a Comment

0 Comments