Ticker

6/recent/ticker-posts

MANCHESTER CITY YAJENGA SANAMU YA DAVID SILVA NA VINCENT KOMPANY ETIHAD


Klabu ya Manchester City imeweza kuwajengea sanamu wachezaji wao waliopita ambao walicheza kwa mafanikio katika klabu hiyo.
Manchester City imewajengea David Silva pamoja na Vincent Kompany sanamu nje ya uwanja wao wa Etihad ili kuwahenzi wachezaji hao.David Silva alijiunga na timu hiyo mwaka 2010 akitokea klabu ya Valencia ya nchini kwao Hispania na kutandika daruga mwaka 2020 kuelekea klabu ya Real Sociadad ya huko huko nchini Hispania ambako mpaka sasa anacheza huko.
Silva ameichezea klabu ya Manchester City mechi 449 na kufunga magoli 81 ligi kuu ya Uingereza na kuisaidia klabu hiyo kubeba kombe la ligi mara 4.
Kwa upande wake Vicent Kompany alijiunga na klabu hiyo mwaka 2008 akitokea Hamburger Sv ya nchini Ujerumani.
Kompany katika kipindi hicho chote ndani ya Manchester City amefunga mabao 18 katika mechi 265 na kuisaidia klabu hiyo kubeba kombe la ligi mara 5

Post a Comment

0 Comments