Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI KALEMANI ATAKA WANANCHI  KUDAI KUPATIWA HUDUMA YA UMEME BADALA YA KUDAI VIFAA VYA KUUNGANISHIA UMEME




Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika kijiji cha Bara kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe uliofanyika Agosti 27,2021.


Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa viongozi wa REA na TANESCO wanaosimamia utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili.


Sehemu ya umati wa wananchi walioshiriki katika Uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani) katika kijiji cha Bara kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe uliofanyika Agosti 27,2021.


Mbunge wa Jimbo la Mbozi,(CCM) Mhe.George Mwenisongole,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika kijiji cha Bara kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe uliofanyika Agosti 27,2021.


Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akikata utepe wa kuzindua Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika kijiji cha Bara kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe uliofanyika Agosti 27,2021.

..........................................................................................................

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ,amewataka wananchi kudai umeme badala ya kudai vifaa vya kuunganishiwa umeme kama vile nguzo, waya na transfoma.

Mhe.Dkt. Kalemani alitoa maelekezo hayo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Mbeya katika kijiji cha Bara Wilaya ya Mbozi uliofanyika Agosti 27,2021.

“Wananchi jukumu lenu ni kudai umeme msijichanganye kuulizia nguzo au kufuatilia nguzo zipo ngapi, idadi ya vifaa haiwahusu. Wajibu wenu ni kulipia fedha za kuunganishiwa umeme na kudai kupatiwa huduma hiyo” amesema Dk.Kalemani

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa, Cosmas Nshenye amesema kuwa shughuli kuu za kiuchumi za Mkoa wa Songwe ni kilimo hivyo wanahitaji umeme kwa ajili ya kusindika mazao ya kilimo ili kuboresha maisha ya wananchi.

“Tunahitaji umeme kwa ajili ya kusindka mazao yanayozalishwa kama vile kahawa na mahindi. Ujio wa umeme utarahisisha utoaji wa huduma za afya, elimu na maji,” amesema Nshenye

Aidha Nshenye amewahamasisha wananchi kuunganisha umeme katika nyumba pamoja na kutunza miundombinu ya kusambaza umeme ,kushirikiana na wakandarasi kwa kuhakikisha wanatoa maeneo yao bila kudai fidia ili kupitisha miundombinu ya kusambaza umeme.

Naye Mbunge wa Mbozi, Mhe. George Mwenisongole ameomba umeme upelekwe katika taasisi zote za elimu, afya, nyumba za ibada, miradi ya maji pamoja na mashine za kukobolea zao la Kahawa.

Post a Comment

0 Comments