Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, alipowasili katika Hfadhi ya taifa ya Ngorongoro kwa ziara ya kikazi |
Na Richard Mrusha
Naibu waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amewasili katika Hifadhi ya Ngorongoro kwa ziara kikazi ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kugawa mizinga ya nyuki 1,500 kwa vikundi vya ufugaji nyuki vilivyoko ndani na pembezoni mwa hifadhi kutoka Wilaya za Karatu na Monduli mkoani Arusha.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo agosti, 13 mwaka huu, Naibu Waziri amekutana na Menejimenti ya NCAA na kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo.
Leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ugawaji wa Mizinga ya Nyuki kwa vikundi vya ufugaji Nyuki ndani na nje ya Hifadhi ili kudhibiti wanyamapori waharibifu, pia atakagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Seneto hadi Kreta na kutembelea Ngorongoro kreta kukagua ikolojia na athari za mimea vamizi.
Aidha, kesho Naibu Waziri huyo, atatembelea eneo la Ndutu linalopendekezwa kujenga mradi wa Faru na mwisho atatembelea maeneo mbalimbali ya Hifadhi kuangalia changamoto ya makazi na shughuli za kibinadamu.
0 Comments