Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI UMMY AMTAKA OCD PANGANI KUWAKAMATA WANAOWAIBIA BAISKELI WATU WENYE ULEMAVU

NAIBU Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye ulemavu) Ummy Nderiamanga akizungumza na watu wenye ulemavu wilayani Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja mwishoni mwa wiki kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo

MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalib Lingo akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga katikati wakati wakishuka kwenye kivuko kuelekea ng'ambo ya pili ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wiaya ya Pangani (DAS) Mwalim Hassani Nyange

MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalib Lingo akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga katikati wakati wakishuka kwenye kivuko kuelekea ng'ambo ya pili ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wiaya ya Pangani (DAS) Mwalim Hassani Nyang


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga katika akiwa kwenye kivuko akivuka ngambo ya pili ya mto Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani PanganiNaibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga katika akiteta jambo na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange kushoto wakatia wa ziara hiyoNA OSCAR ASSENGA,PANGANI

NAIBU Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye ulemavu) Ummy Nderiamanga amemtaka Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) kuhakikisha watu wanaowaibia baiskeli watu wenye ulemavu wanakamatwa na kuchukulia hatua kali za kisheria.

Ummy aliyasema hayo wilayani Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja iliyoambatana na kutembelea maeneo mbalimbali ya watu wenye ulemavu ikiwemo kikundi cha Huruma Disiability na kuzungumza nao kwenye ukumbi wa zamani wa Halmashauri hiyo.

Aisema haiwezekani watu wenye ulemavu wakabuni miradi yao ya kukodisha baiskeli ili waweze kujikwamua kiuchumi huku watu wengine wakikwamisha juhudi hizo hivyo ni lazima washughulikiwe kwa mujib wa sheria zilizopo

“Katika Taarifa ya Mkuu wa wilaya nimesikia hapa kwamba kuna changamoto ya wenye ulemavu wakikopesha baiskeli watu wanaingia mitini Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) naomba watu hao washughulikiwe”Alisema Naibu Waziri Ummy.

Alisema suala hilo analichukulia kwa namna mbili la kwanza ni uonevu na udhalilishaji wa watu wenye ulemavu kwamba hawawezi kukimbia lakini pia wizi kama wizi mwengine hivyo wachukulie hatua kali ili lisiwezi kujitokeza tena kwa sababu leo ni baiskeli kesho wataenda kwa wale wenye migahawa na kuweza kuchukuwa hela zao.

Hata hivyo aliendelea kuwatia moyo na kuwahamasisha watu wenye ulemavu hususani wanafunzi wa kike maeneo ya pwani mambo ya shule yapo nyuma watoto wa kike wenye ulemavu wahakikishe wanasoma kwa bidii lakini pia watumieni mifano hata kama hii ya kwetu wanaweza kufika mbali.

Awali akizungumza wakati akitoa taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Waziri huyo,Mkuu wa wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo alisema changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu ni baadhi yua wateja kutokuwa waaminifu wakikodishwa baiskeli kutokurudisha ikiwemo katika kikundi cha Huruma Disiability kupata hasara ya kuibiwa baiskeli moja na kesi ipo Polisi.

Post a Comment

0 Comments