***********************************
- Awataka Wafanyabiashara kujisikia fahari na uzalendo kulipa Kodi.
- Asisitiza utunzaji wa kumbukumbu ili kurahisisha Zoezi la ukadiriaji wa kodi.
- Achukizwa na Wafanyabiashara wakubwa wanaowatumia Machinga kukwepa Kodi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezindua Kampeni ya usajili wa walipakodi Wapya ikiwa ni utekelezaji wa wa Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuitaka TRA kutanua wigo wa Ukusanyaji wa Kodi.
RC Makalla ametoa wito kwa Wafanyabiashara ambao bado hawajasajili Biashara zao kuzisajili ili Waweze kutambulika na kutimiza takwa la kisheria la ulipaji wa Kodi.
Aidha RC Makalla amewataka Wafanyabiashara kutunza kumbukumbu ili kurahisisha Zoezi la ukadiriaji na ukusanyaji wa Kodi na kuwasisitiza kutoa risiti wanapouza na Wananchi kudai risiti.
Pamoja na hayo RC Makalla ameipongeza TRA Kwa Mapinduzi makubwa Katika ukusanyaji wa kodi Jambo lililowezesha Mapato kupanda na kuwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.
Hata hivyo RC Makalla ameonyesha kuchukizwa na tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa wanaowatumia Wamachinga kukwepa Kodi na kuikosesha Serikali Mapato.
Zoezi la usajili walipakodi Wapya limezinduliwa Mkoa wa Dar es salaam na litatekelezwa Nchi nzima ambapo TRA itakuwa ikitoa namba ya Utambulisho wa mlipakodi (TIN) bure pamoja na Tax clearence kwa Wafanyabiashara Wapya lengo likiwa ni kuongeza Mapato.
0 Comments