Ticker

6/recent/ticker-posts

UJENZI WA MAABARA ZA KISASA ZA USALAMA WA MIONZI WAFIKIA ASILIMIA 85 ARUSHA



Na Alex Sonna,Arusha

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inaendelea na Ujenzi wa awamu ya pili wa Maabara Changamano katika Tume ya Nguvu ya Atomic ambayo itakayo kuwa na Maabara nane na kituo cha usalama wa mionzi na kinga ambapo hadi sasa umefikia asilimia 85.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 13,2021,ambao walifika katika eneo la ujenzi wa mradi huo,Mkurugezi wa Huduma za Tume ya Nguvu ya Atomic Tanzania (TAEC) Edgar Mbaganile amesema mradi huo uligawanyika katika awamu mbili.

Amesema awamu ya kwanza ya mradi huo ambao una maabara nne zinazofanya kazi ulianza kujengwa mwaka 2017 na uliingarimu Serikali shilingi bilioni 2.3.

Mkurugenzi huyo amesema mara baada ya kukamilika mradi huo waliingia mkataba wa pili na TBA wenye thamani ya shilingi bilioni 10.4 ambapo hadi sasa Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imeishatoa shilingi bilioni 6.1 na mradi huo umefikia asilimia 85.

“Huu mradi wa awamu ya pili utakuwa na Maabara nane za kisasa na pia kutakuwa na kituo cha mafunzo ya usalama na kinga ya mionzi,”amesema.

Amesema Tume hiyo imepewa majukumu matatu ambayo ni kusimamia udhibiti na usalama wa kinga ya mionzi,kuendeleza teknolojia ya Nyuklia nchini,kufanya utafiti kwenye masuala ya Nyuklia na kuishauri Serikali.

“Atomic ni mionzi ambayo ina manufaa makubwa ukiangalia katika Hospitali teknolojia inatumika kugundua magonjwa mfano Exray pia katika tiba ya magonjwa mfano Saratani pia viwandani kwenye mifugo na kwenye kilimo,”amesema.

Amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa Nchi kwani wataweza kuongeza uwezo wa kudhibiti matumizi salama ya mionzi pamoja na kuweka mazingira salama kwani kwa sasa teknolojia imepanuka.

“Huu mradi utakuwa na manufaa makubwa sana tutakuwa tumeongeza uwezo wa kuthibiti matumizi salama ya mionzi hivyo wananchi watakuwa salama pamoja na kuweka mazingira salama kwani teknolojia imepanuka sana,tutasogeza huduma kwa wananchi kwani walikuwa wanapata tabu sana.

“Kutakuwa na kituo cha mafunzo wataalamu walikuwa wachache hivyo wataongeza idadi na wananchi wataweza kupata huduma,”amesema.

Alipoulizwa wamejiandaaje kwenye uchimbaji wa madini ya Uranium amesema: “Tumejiandaa vizuri hususani kwenye madini ya Uranium kwani kuna mitambo kwaajili ya kudhibiti mara baada ya madini hayo kuanza kuchimbwa.Mpaka sasa tumeendelea kudhibiti katika chakula Nchi ipo salama,”

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Huduma na Kinga za Mionzi, Yesaya Sungita amesema unapopita uwanja wa ndege kuna vifaa kwa ajili ya mizigo ambavyo vimefungwa mionzi.

“Unapopita uwanja wa Ndege kuna vifaa vya aina mbili kuna kifaa kwa ajili ya mizigo ambacho kinatumia Exray ambayo huwa inamulika mizigo ndani.Mionzi yote inayotumika inapita kwenye mizigo tu na kwenye milango kuna mapazia ndani kuna material ya risasi ili kuhakikisha mtu aliyeweka mzigo asiweze kupata mionzi,”amesema.

Mkurugezi wa Huduma za Tume ya Nguvu ya Atomic Tanzania (TAEC) Edgar Mbaganile,akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika kituo hicho wakati wa ziara ya kuangalia Ujenzi wa awamu ya pili wa Maabara Changamano katika Kituo cha Tume ya Atomic inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ambayo na Maabara nane na kituo cha usalama wa mionzi na kinga.


Mkuu wa Idara ya Huduma na Kinga za Mionzi, Yesaya Sungita,akiwaeleza waandishi wa habari wanapopita uwanja wa ndege kuna vifaa kwa ajili ya mizigo ambavyo vimefungwa mionzi wakati wa ziara ya kuangalia Ujenzi wa awamu ya pili wa Maabara Changamano katika Kituo cha Tume ya Atomic inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ambayo na Maabara nane na kituo cha usalama wa mionzi na kinga.


Mtafiti wa Nuklia Bw.Mujuni Rwemamu,akielezea mashine inayotumika kupimia Mionzi kwa wafanyakazi walio katika mazingira hatarishi.


Mtafiti wa Nuklia Bw.Mujuni Rwemamu,akiangalia mashine wakati akimpima mwaandishi wa habari Mohamed Zengwa kutoka Global Tv Online Mionzi mara baada ya kufanya ziara kuangalia Ujenzi wa awamu ya pili wa Maabara Changamano katika Kituo cha Tume ya Atomic inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ambayo na Maabara nane na kituo cha usalama wa mionzi na kinga.


Fundi Sanifu wa Maabara katika Tume ya Nguvu ya Atomic Tanzania (TAEC) ,akiangalia Mashine inayotumika kupima vifaa vya Mionzi.


Muonekano wa Ujenzi wa awamu ya pili wa Maabara Changamano katika Kituo cha Tume ya Atomic inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ambayo na Maabara nane na kituo cha usalama wa mionzi na kinga.


Waandishi wa habari wakiendelea kukagua Ujenzi wa awamu ya pili wa Maabara Changamano katika Kituo cha Tume ya Atomic inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ambayo na Maabara nane na kituo cha usalama wa mionzi na kinga.


Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukagua Ujenzi wa awamu ya pili wa Maabara Changamano katika Kituo cha Tume ya Atomic inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ambayo na Maabara nane na kituo cha usalama wa mionzi na kinga.

Post a Comment

0 Comments