Mwandishi wa Habari wa TBC Jane John akipata chanjo ya UVIKO 19 leo
Mwandishi wa Habari Zuhura Ally akipata chanjo |
Na John Mapepele, WHUSM
Wanahabari,
wanamichezo na wasanii wameendelea kumiminika leo, Agosti 12, 2021
katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi la
hiari la kupata chanjo ya UVIKO 19. Zoezi hili limeratibiwa na Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya
Afya.
Awali, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi, alifafanua kwamba makundi hayo
yamependekezwa kupewa kipaumbele na Serikali kwa kuzingatia, pamoja na
mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli kwamba kwa mazingira ya
kazi zao, wako katika hatari ya kuambukizwa.
“Zoezi
hili ni la siku mbili Agosti 12-13, 2021 Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar
es Salaam kuanzia saa tatu (03:00) asubuhi, natoa wito kwa wadau wote
kwa hiari yao watumie fursa hii iliyotolewa na Serikali ili wajikinge na
wawakinge wengine na UVIKO-19” ameongeza Dkt. Abbasi.
Dkt.
Abbasi ameendelea kuwasihi wale waliokosa kujiandikisha awali wawe
Wasanii au Wanahabari au Wanamichezo waendelee kuwasiliana kupitia namba
0654063274 au barua pepe matiko.mniko@basata.go.tz ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Amesisitiza kuwa Wasanii walio nje ya Dar es Salaam wataendelea kutumia utaratibu unaoendelea kutangazwa na Wizara ya Afya.
0 Comments