Ticker

6/recent/ticker-posts

CHONGOLO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ANGOLA NCHINI TANZANIA MHE.SANDRO DE OLIVEIRA


Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa Chama cha ukombozi cha MPLA Antonio Lobito. Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akimkaribisha Balozi wa Angola nchini Tanzania Sandro de Oliveira ofisini kwake Makao Makuu ya CCM Dodoma. Tarehe 09 Septemba, 2021. 

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akizungumza na balozi wa Angola nchini Tanzania Sandro de Oliveira, katikati kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mst Ngemela Lubinga, na wa pili kushoto pembeni ya balozi mwenye Kofia ni mwakilishi wa Chama Tawala Cha Angola MPLA Antonio Lobito. 


Katika picha ya pamoja, Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo Katikati, kushoto ni Balozi wa Angola nchini Tanzania Sandro de Oliveira na mwenye kofia nyeusi ni mwakilishi wa Chama tawala cha Angola MPLA Antonia Lobito baada ya mazungumzo leo Makao Makuu ya CCM Dodoma. 

************************* 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amefanya mazungumzo na Balozi wa Angola nchini Tanzania Mhe. Sandro de Oliveira 

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 09 Septemba, 2021 Makao Makuu ya CCM Dodoma, ambapo Balozi aliambatana na mwakilishi wa Chama Tawala cha Angola MPLA Ndg. Antonio Lobito 

Pamoja na mambo mengine, Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Angola, ikiwa ni pamoja na Vyama vya Ukombozi vya CCM na MPLA uliojengwa na waasisi wa Mataifa hayo, Mwalimu Julius Nyerere na Agustino Netho. 

Aidha katika hatua nyingine, Balozi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake wenye maono na wenye kuwajali Watanzania katika kufikia maendeleo ya kweli.

Post a Comment

0 Comments