Ticker

6/recent/ticker-posts

TAIFA STARS YAICHAPA MADAGASCAR MABAO 3-2 KATIKA DIMBA LA MKAPA



Timu ya taifa yya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo wa kufuzu kushiriki kombe la Dunia mwakani baada ya kuinyuka timu ya taifa ya Madagascar mabao 3-2 katiika dimba la mkapa jijini Dar es Salaam.

Dakika ya kwanza tu mpira unavyoanza Taifa Stars ilifanikiwa kupata penati baada ya Simon Msuva kuchezewa rafu mbaya na kipa wa madagascar akijaribu kuokoa shambulizi la kushtukiza.

Penati ilipiga na Erasto nyoni na kufanya ubao uusomeke 1-0 Taifa Stars kuongoza. Dakika ya 26 Novatus Dismas alifanikiwa kufunga bao zuri na kufanya Taifa Stars kuongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 36 Rakotohoharimala kupachika bao na baadae Fontaine kuisawazishia timu yake ya taifa na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 2-2.

Kipindi cha pili timu zote zilikuwa zinahitaji ushindi katika mchezo huo ambapo walikuwa wanafanya mashambulizi ya kushtukiza kwa timu zote mbili.

Feisal Salumu aliibuka shujaa dakika ya 52 baadaa ya kupachika bao zuri akipokea pasi murua kutoka kwa mshambuliaji Mbwana Samata na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments