Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA NBC KUDHAMINI LIGI KUU TANZANIA BARA, YASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU


Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi na rais wa TFF Wallace Karia wakisaini mkataba wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu wenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bw. Theobald Sabi na Rais Wa TFF Bw. Wallace Karia wakizindua logo rasmi itakayotumika kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara. Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi rais wa TFF Wallace Karia wakionesha mkataba wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu wenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 uliosainiwa leo.

********************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirikisho la Soka Tanzania limesaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini wa Ligi kuu soka Tanzania bara na Benki ya NBC Tanzania ambapo kwa msimu wa 2021-22 ambao tayari unaendelea watadhamini kwa jumla ya shilingi Bilioni 2.5 bila VAT.

Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ngazi ya mpira wa miguu ilikuwa imeanza kutimua vumbi papokuwa na mdhamini wa ligi hiyo hivyo basi sasa ligi hiyo itakuwa NBC PREMIER LEAGUE kwa mismu mitatu mfululizo.

“Mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo unaofuatiliwa sana hapa nchini. Hata vipindi vya michezo ni vingi zaidi, hivyo Ligi kuu ni miongoni mwa ligi bora barani Afrika kwa mujibu wa CAF na sisi tuko namba 8“ Bw. Theobald Sabi (Mkurugenzi Mtendaji wa NBC)

Post a Comment

0 Comments