Ticker

6/recent/ticker-posts

BWALYA AIPA USHINDI SIMBA SC, YAICHAPA 1-0 POLISI TANZANIA*****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Simba imefanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC mara baada ya kuwafunga Polisi Tanzania bao 1-0 katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao timu zote zilikuwa zinashambulia kwa kushtukiza walikwenda mpaka mapumziko timu zote zikiwa hazijapata kitu.

Polisi Tanzania ambayo imeanza ligi vizuri ambapo mechi zake zote tatu ilifanikiwa kupata ushindi na kuweza kuongoza ligi hiyo ambayo kwasasa imekuwa ya ushindano haa kutokana na timu zote kuonekana kujiandaa ipasavyo.

Simba Sc ilifanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa ambapo ilizaa matunda kwani kuingia kwa Benard Morrison kulionesha timu kuhitaji muda wote kupata goli hasa kwa kulisakama goli la wapinzani kwa nguvu.

Morrison alichezewa rafu dakika ya 86 ya mchezo hivyo mwamuzi akaamuru kuwekwe mkwaju wa penati ambao ulienda kupigwa na kiungo Mzambia Larry Bwalya na kuiwezesha ttimu yake kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments