Ticker

6/recent/ticker-posts

DC MBONEKO AONGOZA WANANCHI,VIONGOZI KUCHIMBA MSINGI UJENZI KITUO CHA AFYA IHAPA OLD SHINYANGA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.

******************************


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amewaongoza wananchi na viongozi kuchimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.


Zoezi hilo la uchimbaji msingi lililofanyika leo Jumamosi Oktoba 16,2021 limefanywa pia na Wakuu wa Idara Manispaa ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaari Mrisho Satura pamoja na viongozi na wananchi wa kata ya Old Shinyanga.


Mboneko amewapongeza viongozi wa kata ya Old Shinyanga wakiongozwa na Mhe. Diwani Enock LIeta na mwenyekiti wa CCM kata Mhe. Mwanaidi Abdul, wenyeviti wa vijiji na Makamanda wa Jeshi la jadi (sungusungu )kwa kuhamasisha wananchi kushiriki kuchimba msingi wa kituo cha afya Ihapa ili kuondoa adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.


"Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kiasi cha shilingi Milioni 250, fedha hizi zingeweza kupelekwa kwenye kata nyinyine yoyote lakini imechaguliwa kata ya Old Shinyanga. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mhe. Rais Samia kwa sababu katika awamu yake hii ya sita, alituletea milioni 50 kwa ajili ya kukamilisha pale zahanati na ameongeza shilingi milioni 250 kwa sababu ameona wananchi wa Old Shinyanga Ihapa wanafanya kazi vizuri lakini wanajitoa sana kuunga mkono juhudi za serikali",amesema Mboneko.


“Kwa hiyo Shilingi Milioni 250 ni ajili ya ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) na Maabara na zitakuja tena shilingi milioni 250 zingine ili kuhakikisha huduma zinakamilika katika kituo cha afya Ihapa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la akina mama na mtoto. Mhe. Rais ameangalia suala la huduma za afya kwa wananchi na zaidi sana suala la akina mama na watoto,akina mama wanapata tabu sana kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya”, ameongeza.


Mkuu huyo wa wilaya pia amewashukuru wananchi wazalendo waliotoa maeneo yao ili huduma za afya ziweze kupatikana Ihapa na wananchi wamechanga kiasi cha shilingi milioni 6.5 ambapo Mkurugenzi amesema kama kuna gharama zitabakia ataongezea fedha kwa ajili ya ujenzi huo ili eneo liwe kubwa ambao sasa majengo yapo kwenye hatua za awali.


"Tunamshukuru Mhe. Rais Samia, walau sisi katika wilaya ya Shinyanga tunabakiza tarafa moja ambayo haina kituo cha afya ambayo ni Ibadakuli lakini kwa kuwa tunajua jinsi Mhe. Rais alivyomsikivu atatuletea pia fedha kwa ajili ya kituo cha afya Ibadakuli",amesema Mboneko.


Amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano akisema ushirikiano na mshikamano uliopo baina ya serikali,chama na wananchi mambo yote yatakwenda vizuri na kuhakikisha mipango mizuri inayopangwa katika wilaya ya Shinyanga inafanikiwa na miradi kukamilika kwa wakati kama serikali inayoelekeza.


"Hakikisheni mnatunza miundo mbinu itayojengwa hapa, na niwahakikishie kuwa katika kituo cha afya Afya Ihapa hatuna changamoto ya maji wala umeme…lakini nitawaomba TARURA waweze kuimarisha barabara ili kituo hiki kiweze kupitika na kufikika kirahisi",amesema.


Aidha amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga na Wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa kituo cha afya Ihapa kukamilisha ujenzi kwa wakati, ubora na gharama nafuu.


“Hakikisheni ujenzi wa kituo hiki cha afya unakamilika kwa wakati,ubora na chenji ibaki. Nataka Shinyanga tuwe wa mfano, mimi kwenye Wilaya yangu huwa sipendi kushindwa,napenda mambo yafanyike vizuri”,amesema Mboneko.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaari Mrisho Satura ameahidi kukamilisha ujenzi wa miradi bora kwa gharama nafuu.


Diwani wa kata ya Old Shinyanga Mhe. Enock Charles Lieta amesema wananchi wa eneo hilo wataendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika utekelezaji wa miradi na kwamba watahakikisha wanasimamia vizuri ujenzi wa kituo cha afya Ihapa ikiwa ni pamoja na kuzuia mianya ya wizi wa fedha na uharibifu wa miundombinu.


Naye Mwenyekiti wa Jeshi la Jadi Sungusungu wilaya ya Shinyanga, Jiganza Jidula amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwa hamasa yake kwa wananchi kushiriki kwenye ujenzi wa miradi huku akiwasihi wananchi kuendelea kuunga mkono serikali kwa shughuli mbalimbali.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihapa, Lucas Basu amesema kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya Ihapa kutaondoa adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu zaidi ya kilomita 12 kufuata huduma za afya Mjini Shinyanga katika kituo cha afya Kambarage.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza leo Jumamosi Oktoba 16,2021 katika eneo Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza leo Jumamosi Oktoba 16,2021 katika eneo Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katika eneo Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga. Kushoto aliyevaa Truck Suit ya kijani ni Diwani wa kata ya Old Shinyanga Mhe. Enock Charles Lieta.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga. Kushoto aliyevaa Truck Suit ya kijani ni Diwani wa kata ya Old Shinyanga Mhe. Enock Charles Lieta.
Wananchi na viongozi mbalimbali wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza jambo kwenye eneo la Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaari Mrisho Satura
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaari Mrisho Satura (kulia) akimhakikishia Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwa atakamilisha Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Wananchi na viongozi mbalimbali wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Wananchi na viongozi mbalimbali wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaari Mrisho Satura
akizungumza wakati viongozi na wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.


Diwani wa kata ya Old Shinyanga Mhe. Enock Charles Lieta akizungumza wakati viongozi na wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Diwani wa Viti Maalumu Pika Chogero akizungumza wakati viongozi na wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Old Shinyanga Mhe. Mwanaidi Abdul akizungumza wakati viongozi na wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihapa kata ya Old Shinyanga, Lucas Basu akizungumza wakati viongozi na wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.


Mwenyekiti wa Jeshi la Sungusungu wilaya ya Shinyanga, Jiganza Jidula akizungumza wakati viongozi na wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya kumbukumbu na Wahandisi wanaosimamia Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara katika kituo cha afya Ihapa kilichopo kata ya Old Shinyanga.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments