Ticker

6/recent/ticker-posts

PSSSF YASHIRIKI HAFLA YA UPANDAJI MITI, DODOMA

* Watanzania tunaamini katika kilimo na Uchumi wa Kijani


* Kushiriki kupanda miti ni tukio muhimu sana kwetu, ni wajibu wetu kuyalinda mazingira

PSSSF imeungana na Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda katika kampeni maalum ya kuhamasisha upandaji miti mkoani Dodoma inayoratibiwa na Habari Development Association.

Akizungmza katika hafla hiyo Waziri Mkuu mstaafu Mh. Mizengo Pinda alisema “sisi watanzania tunaamini katika kilimo na uchumi wa kijani hivyo ni lazima tupande miti ya kutosha ili tutunze mazingira na kupata mafanikio katika kilimo”.

Hafla hiyo imefanyika leo Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Viongozi wa CCM mkoa, Mbunge wa Dodoma Mjini, Watendaji mbalimbali wa Serikali, walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Nala na watumishi wa Mfuko wa PSSSF.

Ujumbe wa PSSSF uliongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSSSF, Bibi Beatrice Musa Lupi ambaye naye alipanda miti kuashiria utayari wa Mfuko kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Taasisi ya Habari Development Association katika kampeni ya kuufanya Mji wa Dodoma kuwa wa Kijani.

Akizungumza katika hafla hiyo Bibi Lupi alisema, PSSSF ni sehemu ya jamii ya Dodoma na hivyo basi Mfuko una wajibu wa kuhakikisha unashiriki katika shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kupanda miti ili kuyalinda mazingira. Alibainisha kwamba Mfuko unafahamu faida ya upandaji miti na umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kwa ustawi wa jamii ya wana Dodoma.



Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza wakati wa halfa ya upandaji miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Mhe. Jabir Shehekimweri akizungumza wakati wa halfa ya upandaji miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma


Mkurugenzi wa Fedha wa PSSSF, Bi. Beatrice Musa Lupi akizungumza wakati wa halfa ya upandaji miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza wakati wa halfa ya upandaji miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma
Katibu wa Taasisi ya Habari Development, Bernard Mwanawile akizungumza wakati wa halfa ya upandaji miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda, akipanda mti pamoja na Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Beatrice Musa Lupi wakati wa hafla ya upandaji miti katika shule ya Sekondari Nala, Dodoma. Nala, Dodoma



Wanafunzi Pamoja na walimu na wageni waalikwa (picha ya chini) katika hafla ya upandaji miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma, Oktoba 16, 2021.


Post a Comment

0 Comments