Ticker

6/recent/ticker-posts

FARU KUONGEZWA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI


Kamishina Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Bw.Mathew Mombo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi hivi karibuni .

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kutokana na tafiti zilizofanywa na kugundulika kuwa mnyama aina ya faru alikuwepo katika hifadhi ya taifa Mikumi hapo mwanzo, Uongozi wa hifadhi hiyo wameamu kufanya utaratibu wa kumrudisha mnyama huyo ili kuwepo na idadi kamili ya wanyama wakubwa watano .

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi amesema miaka ya nyuma hifadhi hiyo ilikuwa moja kati ya maeneo ambayo ilikuwa na faru ambaye ni mnyama wa tano kukamilisha idadi ya wanyama wakubwa watano.

"Kwasababu ilikuwepo fursa hii basi itakuwa sio mbaya tukianzisha mchakato wa kuweza angalau kama itawezekana kumrudisha mnyama huyo ili kukamilisha idadi ya wanyama watano wakubwa ambao kwa ujumla wake inakamilisha ile haja na matakwa ya wageni kutaka kuona wanyama watano ndani ya sehemu moja". Amesema

Amesema endapo watafanikisha zoezi hilo basi idadi ya wageni wa ndani na nje ya nchi wataongezeka ili kuona hao wanyama wakubwa (Big Five) ambao wanapatikana nchini Tanzania.

Aidha amesema Hifadhi ya Taifa ya Mikumi inafanya tafiti mbalimbali ikiwemo maeneo yanayotembelewa na tembo ili wanapofanya tafiti watakuja kugundua kwamba kumbe kuwafuatilia wanyama hao ni rahisi kwakujua maeneo wanayoyapenda kuyatembelea nje ya hifadhi kupunguza zile adha na athari ambazo wanawapatia wananchi wanaozunguka Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Amesema imekuwa ni changamoto kubwa kwa wanyama wakubwa kama tembo kuharibu na kujeruhi wakazi ambao wapo karribu na hifadhi ya Taifa ya Mikumi hivyo kuna umuhimu wa kufanya tafiti kuwezesha kudhibiti uvamizi na uharibifu wa mali za wakazi.

Post a Comment

0 Comments