Ticker

6/recent/ticker-posts

FEET TANZANIA YAZINDUA MRADI WA UHAMASISHAJI WA MTOTO WA KIKE KUPENDA SOMO LA SAYANSI



Mratibu wa FEET Tanzania Bw.Alfred Kiwuyo akiwa pamoja na baadhi ya Wanafunzi wa shule za Sekondari akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa STEM unaolenga kuhamsisha watoto wa kike walioko shule za Sekondari kupenda somo la Sayansi. Uzinduzi umefanyika leo Jijini Dar es Salaam. Mratibu wa FEET Tanzania Bw.Alfred Kiwuyo akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa STEM unaolenga kuhamsisha watoto wa kike walioko shule za Sekondari kupenda somo la Sayansi. Uzinduzi umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Temeke Bi.Ahlam Hamad akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa STEM unaolenga kuhamsisha watoto wa kike walioko shule za Sekondari kupenda somo la Sayansi. Uzinduzi umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Temeke Bi.Donatila Thomas akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa STEM unaolenga kuhamsisha watoto wa kike walioko shule za Sekondari kupenda somo la Sayansi. Uzinduzi umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Temeke Bi.Noela Massawe akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa STEM unaolenga kuhamsisha watoto wa kike walioko shule za Sekondari kupenda somo la Sayansi. Uzinduzi umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Juhudi Ndg.Said Rajab akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa STEM unaolenga kuhamsisha watoto wa kike walioko shule za Sekondari kupenda somo la Sayansi. Uzinduzi umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa FEET Tanzania Bw.Alfred Kiwuyo akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafuunzi wa Sekondari mara baada ya kuzindua mradi wa STEM unaolenga kuhamsisha watoto wa kike walioko shule za Sekondari kupenda somo la Sayansi. Uzinduzi umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************************

Katika kusheherekea Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, TAASISI ya FEET Tanzania imezindua Mradi maalumu uliopewa jina la STEM kwa lengo la kuhamasisha watoto wa kike walioko katika Shule za Sekondari nchini kupenda masomo ya sayansi huku ikieleza kupitia mradi huo shule za sekondari 100 zitashindana kupata wanafunzi wa kike watakaokuwa na mawazo na maoni mapana kuhusu masomo ya sayansi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam ,Mratibu wa FEET Tanzania Bw.Alfred Kiwuyo amesema taasisi yao ambayo siyo ya kiserikali imeamua kuzindua mradi huo ambao utakwenda hadi Desemba 11 mwaka huu na kisha kumalizika kwa tukio kubwa la kutoa zawadi kwa sekondari bora na wanafunzi bora katika masomo ya sayansi.

"FEET Tanzania tumejikita katika kusaidia elimu kwa mtoto wa kike , usawa wa kijinsia pamoja na kuuhisha ushiriki wa vijana katika masuala ya mazingira.Nia yetu kubwa ni kuboresha mazingira rafiki ya mtoto wa kike kwenye jamii, pamoja na kuzingatia usawa katika elimu.

"Leo Oktoba 11 tuko hapa kuzindua programu ya STEM inayohusu watoto wa kike kupenda masomo ya sayansi, tumegundua katika masomo ya sayansi watoto wa kike wameachwa nyuma sana, hata katika ripoti ya BEST mwaka 2016 inaoesha ufaulu wa watoto kike kwenye masomo ya sayansi umekuwa mdogo , pia uelewa wao umekuwa mdogo, hivyo tumeona tuje na mradi huu wa kuhuhisha masomo ya sayansi ili mtoto wa kike apende kusoma, pia kuangalia namna gani tunaweza kuongoza ufauli wa mtoto wa kike katika masomo ya sayansi,"amesema.

Amefafanua mradi huo wa STEM umejikita katika masuala sayansi, teknolojia , Uhandisi na hesabu na lengo ni kumsaidia mtoto wa kike."Mradi huu unakwenda kumfanya mtoto wa kike kuwa karibu na kupenda zaidi masomo ya sayansi kwa kubuni project ambazo zitakuwa na tija.

"Tumezindua mradi huu leo Oktoba 11 na itakwenda mpaka Desemba 11 ambapo wanafunzi wa kike watatengeneza project za kisayansi, mawazo mapana katika sayansi, na tutatoa zawadi kwa shule bora na watoto bora wa kike watakaokuwa wameleta mawazo mazuri ya kisayansi watazawadia vifaa vya maabadara na vitabu vya masomo ya sayansi, lengo ni watoto wa kike kupenda sayansi,"amesema.

Kiwuyo amesema kauli mbiu ya Siku ya Mtoto wa kike inaweka wazi namna ya kumsaidia mtoto wa kike kupenda masomo ya sayansi na katika kuuhisha teknolojia kwa mtoto wa kike, hivyo FEET wameona waje na mradi huo.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Temeke anayechukua mchepua wa masomo ya sayansi Ahlam Hamad amesema FEET Tanzania wamefanya jambo kubwa kuja na mradi huo na wanaamini utakwenda kuongeza chachu wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi.

"Watoto wa kike tumekuwa nyuma sana kuingia katika miradi inayohusu sayansi , kwasababu tofauti tofauti ikiwemo ya kutokuwepo kwa muongozo ambao unahusu watoto wa kike , kuna changamoto ya uhaba wa walimu wa sayansi,"amesema.

Wakati huo huo Mwanafunzi wa Shule ya sekondari Temeke Noela Massawe ametoa ombi kwa Serikali kama kuna uwezekano iweke mikakati ya kuanzisha programu za kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya sayansi, pia iongeze walimu ambao watasaidia watoto wa kike kusoma sayansi.

"Sio watoto wote wa kike hawapendi kusoma sayansi bali wakati mwingine kuna changamoto zinazosababisha kushidwa kusoma , kwa mfano unakuta mtoto wa kike anapenda kusoma sayansi lakini mazingira ya nyumbani yanamkwamisha."

Kwa upande Mwanafunzi Donatila Thomas wa kidato cha tano sekondari ya Temeke amesema anawashauri wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi kwani ni mazuri na yana ajira zinazoeleweka na kwamba Serikali inatoa kipaumbele zaidi kwa watoto wa kike wanaopenda sayansi.

"Masomo ya sayansi yana ajira nyingi, watoto wa kike wasome kwa bidii kwani hata Serikali inatoa kipaumbele, hivyo niwatoe hofu wanafunzi wa kike kuhusu msomo ya sayansi, ni masomo ya kawaida na sio magumu kama ambavyo wengi wamekuwa wakituminisha, kikubwa tujiamini na tunaweza,"amesema.

Mwanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Juhudi Said Rajab amesema wameamua kuungana na FEET Tanzania kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa mradi wenye nia njema na mtoto wa kike kuhakikisha anapenda masomo ya sayansi."Ushauri wangu kwa watoto wa kike wajitahidi kusoma masomo ya sayansi na sio tu kwa ajili ya kujinufaisha wa o peke yao bali wanufaishe na jamii kwa ujumla,"amesema Rajabu.

Post a Comment

0 Comments