Ticker

6/recent/ticker-posts

HOSPITALI YA HEAMEDA NA MADAKTARI BINGWA WA HOSPITALI YA APOLO WATOA HUDUMA ZA AFYA BURE


Daktari wa macho, akimuhudumia mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Heameda kupata huduma ya afya ya macho katika hospitali hiyo, Bunju B, Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Hospitali ya Heameda, Daktarii Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Hery Mwandolela, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Apolo ya India, ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 11 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo, iliyoko Bunju B, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.Kushoto ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Apolo ya nchini India Venkatesh T.M

Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Heameda, wakitoa huduma kwa wananchi waliofika kupima afya zao bure, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 11 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo, iliyoko Bunju B, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

****************************

Na Mwandishi Wetu

HOSPITALI ya Heameda ya Bunju B na madaktari bingwa wa Hospitali ya Apolo ya India wameamua kutoa huduma za afya bure kwa wananchi wa Dar es Salaam na mikoa jirani wakati wa hospitali hiyo inaposherehekea maadhimisho ya miaka 11 tangu ianze kutoa huduma za matibabu ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Henry Mwandolela, amesema wameamua kufanya vipimo na matibabu bure kama kurudisha kwa jamii wanaowahudumia kila siku.

Dk.Mwandolelea amesema kila ifika Oktoba 20 ya kila mwaka wamekuwa wakiadhimisha siku ya kuanzishwa kwa hospitali kwa kutoa huduma ya vipimo bure kwa wananchi wote katika magonjwa yasioambukiza yakiwemo maradhi ya kisukari, shinikizo la damu.

"Tumeshirikiana na Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo, upasuaji uti wa mgongo na ubongo, mwingine ni bingwa wa upasuaji wote kutoka katika hospitali ya Apolo nchini India, wote wamekuwa wakitoa huduma na tumefanya hivyo ili kurudisha kwa jamii", amesema.

Dk.Mwandolela amesema hospitali hiyo sasa imeimalika katika kutoa huduma kutokana na kuwa na vipimo vya kisasa, pia wamekuwa wakitoa huduma za majumbani na oparesheni mbalimbali, hivyo wananchi waje wapate huduma.

Ameongeza kuwa lengo la kushirikiana na wataalamu hao kutoka nchini India katika Hospitali ya Apolo ni pamoja kuimarisha ushirikiano wao na kubadirishana utaalamu kwani kuna baadhi ya vitu wao wanavijua na vingine hawavijui, watajifunza kutoka kwetu."Tumeanza kutoa huduma ya vipimo bure kwa wananchi kuanzia Oktoba 18 na tutaendelea hadi Oktoba 20,2021 ambayo ndio siku tuliyoanza kutoa huduma miaka 11 iliyopita."

Kwa upande wa mwananchi aliyepata huduma katika hospitali hiyo ni, Mkazi wa Mbezi Luisi, Bupe Kanafunzi, amesema anaifahamu hospitali hiyo tangu ilipokuwa kliniki kule Upanga na sasa ni hospitali, wameendelea kuwa na huduma bora za matibabu.

Bupe amesema wana madaktari bingwa kwa watoto na wanawake na magonjwa mengine kwani wanatoa huduma nyingi kwa uhakika na uaminifu bila usumbufu wowote.

"Nikweli nimepata huduma hapa ya macho nimepimwa na nimepewa miwani mipya, wananchi wenzangu waje wapate huduma, hii hospitali ni wakweli kwani madaktari bingwa kutoka India katika Hospitali ya Apolo wapo na wanaendelea kutoa huduma na huduma zote muhimu zinapatikana", amefafanua.

Mwananchi mwingine Mzee Dastan Mrutu, amesema amekuwa akitibiwa hapo tangu mwaka 2008, yeye ni mgonjwa wa 50 kati ya wagonjwa 10,000 wanaopita katika mikono ya Dk. Mwandolelea.

Amesema ni fahari kubwa kwa kijana wa Kitanzania kuendesha hospitali kubwa ya Kimataifa kama hiyo, pongezi sana kwake kwani naamini anazijua shida za Watanzania ndiyo maana amefanya uwekezaji mkubwa ili kuokoa maisha maisha ya Watanzania.

Mrutu ameongeza amekutana na watalaamu kutoka India kuja kupata huduma za afya, kwani kuja kwao hapo ni kubadilishana uzowefu wa kazi na elimu mpya ya taaluma katika hospitali ya Heameda, ambayo imekuwa ikitoa huduma za kibingwa na magonjwa ya kawaida.

"Hili wazo la kushirikiana madkatari bingwa kutoka nje ni zuri sana, zamani hata ukiwa na ugonjwa wa kawaida utapelekwa India, wakati inawezekana wakaletwa madaktari bingwa na Maprofesa wakatoa huduma za kibingwa hapa hapa bila kutumia gharama kubwa kwenda huko", amesema.

Amesema kwakuwa vipimo vya kisasa vipo hapa hapa nchini, hakuna haja ya kujazana katika ndege kwenda kutibiwa nje ya nchi, hao wataalamu waletwe hapa tupate huduma kama inavyofanya hospitali Heameda.

"Matibabu katika hospitali hii yanakidhi kwa kiwango kikubwa kwani hakuna urasimu kuanzia kwa madaktari hadi kwa wauguzi, ndiyo maana huduma zao zinaenda haraka na bora na hakuna mrundikano wa wagonjwa."

Post a Comment

0 Comments