Ticker

6/recent/ticker-posts

MIONGOZO ADA ZA UKUSANYAJI TOZO ZA UMWAGILIAJI WAKAMILIKA



Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Dodoma kuhusiana na uchangiaji wa Tozo katika sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji.

***************************

Na; MwandishiWetu– Dodoma

kutekeleza agizo la Serikali linalowataka wakulima wote wanaojishughulisha na shughuli za kilimo cha umwagiliaji kuachangia asilimia tano katika mfuko wa maendeleo yakilimo cha Umwagiliaji, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekamilisha Miongozo kanuni nataratibu za ukusanyaji wa tozo za Kilimo cha Umwagiliaji.

Hayo yamesemwa Mapema Leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake.

Bw. Kaali alisema mapema mwezi July Mwaka huu Serikali kupitia Waziri wa Fedha ilitoa agizo la wakulima waliopo katika skimu za kilimo cha umwagiliaji kuchangia asilimia tano kwa kila hekta na fedha hizi ziingizwe katika mfuko wa umwagiliaji kwaajili ya kugharamia matunzo, matengenezo pamoja na uendeshaji wa skimu za kilimo cha umwagiliaji.

Aidha Mkurugenzi Kaali amesema kuanzia mwezi huu wa kumi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaanza kampeni maalumu ya kutoa elimu kuhamasisha wananchi mbalimbali wachangie watoe hizi ada kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji,

“Hivyo watumishi mbalimbali kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na viongozi mbalimbali wa serikali watakwenda katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kuelemishana kuhamasisha utoaji wa ada hizi za umwagiliaji.” AlisemaKaali

Bw. Kaali wamewaasa wakulima wanaojihusisha na kilimo cha Umwgiliaji kuchangia ada za umwagiliji kwani amesema ni fursa nzuri sana ambayo imetolewa na Serikali kuchangia fedha katika mfuko wa umwagiliaji ili kuweza kutatua changamoto kubwa katika skimu mbalimbali hapa nchini.

Kwa u pande wakeKaimu Mkurugenzi uendeshaji Bwana Enterbet Nyoni amesema katika skimu za kilimo chaumwagiliaji zisozendelezwa mgawanyo wa Ada yatozo ya asilimia tano ya tozo,utahusisha asilimia sabini na tano (75%)kubakiakatikaskimuhusikanaasilimiaishirininatano (25%) itakwendakatikamfukowamaendeleoyakilimo cha umwagiliaji.

Post a Comment

0 Comments